TAASISI ya Saratani ya Hospital ya Ocean Road leo imefanya matembezi ya hisani kwa lengo la Kuhamasisha na kuchangia zaidi ya milioni 120 zinazohitajika kwa ajili ya kununua vifaa tiba vya chemotherapy.

Matembezi hayo yalianzia Hospitali ya Ocean road na kumalizika hapo hapo huku wakizunguka moja ya barabara za jiji la Dar es Salaam huku Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Hamis Kigwangala akiwa ni mgeni rasmi.
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Hamis Kigwangala akizungumza mara baada ya kumaliza matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa saratani ya matiti yaliyoandaliwa na Taasisi ya Saratani ya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ambapo huu ni mwaka wa nne tokea yameanzishwa. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Mmoja ya wagonjwa ambaye amepona saratani ya matiti akitoa ushuhuda mbele ya wageni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...