THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM: KUANZA KWA MUHULA/MWAKA WA MASOMO 2016/17

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) anawatangazia kuwa Muhula wa kwanza wa Mwaka wa Masomo 2016/2017 utaanza rasmi tarehe 7/11/2016.  Wanafunzi wote wa Mwaka wa kwanza (OD & BEng / BTech) wanatakiwa kuripoti chuoni kuanzia siku ya Jumamosi tarehe 29/10/2016 kwa usajili na “Orientation Week” itakayofanyika kwa wiki moja kuanzia tarehe 31/10/2016. Aidha, mambo yafuatayo ni muhimu sana kuzingatiwa kwa wanafunzi wote kuelekea ufunguzi wa Chuo.

1. Usajili utafanyika kwa wiki mbili tu na mwanafunzi ambaye hatakamilisha usajili wake kwa muda huo hataruhusiwa kuingia darasani.

2. Ili mwanafunzi akamilishe usajili ni lazima alipe Ada na kuwasilisha Bank pay in slip wakati anasajiliwa.

3. Wanafunzi wa Stashahada wenye ufadhili binafsi (Private sponsored Students) watakaopata nafasi ya  Malazi katika mabweni ya Taasisi watalazimika kulipa jumla ya Tshs 990,000/- kwa mwaka na watahudumiwa kwa utaratibu maalum watakaoelekezwa baada ya kukamilisha malipo hayo.

4. Kila mwanafunzi wa mwaka wa kwanza atahitajika kuwasilisha vyeti halisi wakati wa usajili kinyume cha hapo hatasajiliwa kama mwanafunzi wa DIT.

5. Sheria zote za udahili na mitihani zitazingatiwa kama zilivyochapishwa katika Prospectus ya Taasisi kwa Wanafunzi wote wanaoendelea yaani mwaka wa Pili hadi wa Nne na KWA WANAFUNZI WAPYA WANAONZA MWAKA WA KWANZA 2016/2017 kuna nyongeza kwenye sheria hizo kwamba; Mwanafunzi atakayeshindwa  kufaulu CA (Continous Assessment) hatapewa nafasi ya mtihani wa Marudio yaani Supplementary Exam na badala yake atalazimika kuirudia hiyo “module” upya katika mwaka wa kimasomo unaofuata. 

6. Akaunti zifuatazo zitatumika kwa malipo.
Ada na gharama nyingine:  A/C. No. 0150408417800 – CRDB
Chakula na Malazi; Bima ya Afya (NHIF); DITSO Fees zilipwe zote kupitia 
A/C No. 011103005481 – NBC LTD Tawi lolote kabla ya Usajili.

7. Malipo ya Ada ni lazima yalipwe kwa angalau 50% kabla ya kujisajili.

Ofisi ya Uhusiano,
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam,
S.L.P 2958,
Dar es Salaam.