Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii
Chama cha wafanyakazi wa migodini na kazi za ujenzi (TAMICO), kimewataka
wadau na wafanyakazi ambao wanafanya kazi katika mashirika ya ujenzi
kujiunga na chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa
TAMICO Taifa,Mhandisi Fred Kapamila,amesema kuwa matokeo ya huru na
utandawazi ni ajira isiyo na staha kwasababu makampuni yanawania kupata
faida zaidi kupitia kuwapunja wafanyakazi wao.
"Tarehe 18/10/2016 chama kilifanya mkutano wake mkuu na kupata safu ya
viongozi wapya hivyo uongozi mpya unawaomba watu wenaofanya kazi katika
makampuni ya migodi kujiunga kwa wingi katika chama hicho hili waweze
kupata msaada pindi wanapopata matatizo"amesema Kapilima.
Amesema kuwa uongozi mpya umejitayarisha vya kutosha kupambana na
changamoto za kuhakikisha dhamira na matarajio ya wanachama yanafikiwa
katika kipindi kijacho cha miaka mitano.
Alitoa wito kwa serikali kuangalia upya maslahi ya wafanyakazi wa migodini ambao wamekuwa wakiteseka kila kukicha.
Mwenyekiti wa wa chama cha wafanyakazi wa Migodi,Nishati,ujenzi na kazi
nyinginezo nchini,TAMICO,Mhandisi Fred Kapimila,akizungumza na
Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni katibu wa chama
hicho, Thomas Sabai,kushoto Afisa elimu na mafunzo Philotea
Ruvumbagu,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...