THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TANESCO YATILIANA SAINI MIKATABA YA KUJENGA NJIA YA UMEME WA KILOVOTI 400.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania, (TANESCO), Felchesmi Mramba, (kushoto), akibadilishana hati za mkabata na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton baada ya kusini, mradi wa ujenzi wa njia ya umeme (transmission line) itakayounganisha Tanzania na Kenya, makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2016. Shirika hilo limeingia mkataba na makampuni matatu kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa Msongo wa KV400 unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya dola za Kimarekani
309.26

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said.
SHIRIKA la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), limesaini mkataba na makampuni matatu kujenga njia ya umeme, (Transmission lines), wa Msongo wa Kilovolti 400 utakaounganisha Tanzania na Kenya.

Hafla ya kutiliana saini mikataba hiyo, imefanyika leo Oktoba 7, 2016 makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, ambapo Shirika hilo la Umeme linalomilikiwa na serikali, limetiliana saini mikataba hiyo na makampuni ya Bouygues Energies Service, Energoinvest na Kalpa-Taru.

Akizungumz wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Felchesmi Mramba, alisema, Ujenzi wa Mradi huu wenye urefu wa Kilomita 414, utaanzia Mkoani Singida,-Babati-Arusha hadi Namanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.

Kisha Mradi utaunganishwa na njia ya Msongo wa Kilovolti 400 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka eneo la Isinya, Nairobi, nchini Kenya hadi eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya, (Namanga) ambapo utaunganisha na njia ya umeme wa wa Msongo wa Kilovolti 400kv kwa upande wa Tanzania.

“ Napana niwahakikishie, kuwa huu ni mfululizo wa miradi mikubwa inayotekelezwa na TANESCO na utawezesha usafirishaji wa umeme wa Mgawati 2000 katika pande zotekenya na Tanzania”. Alifafanua Mramba.

Akifafanua zaidi, Mhandisi Mramba alsiema, utekelezaji wa mradi huu unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni 309.26 utakamilika katika kipindi cha miezi 24, sawa na miaka 2.
Kusoma zaidi bofya HAPA.