Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila amesema Tanzania ijiandae kunufaika kibiashara na kukuza uchumi wa Taifa na mtanzania mmoja mmoja ifikapo mwakani kwa sababu wapo mbioni kuingia kwenye orodha ya nchi ambazo biadhaa zake za chakula zitawekewa nembo ya Halal ambapo bidhaa hizo zitauzwa kwa nchi 33 kimataifa ikiwemo Malaysia inayotoa nembo ya JAKIM.

Halal ni nembo ambayo inawekwa katika bidhaa inapoazalishwa hadi kumfikia mlaji kwa kuzingatia viwango maalum vilivyowekwa na kampuni ya JAKIM nembo ya halali.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Lolila amesema nembo ya Halal itaweza kumhakikishia mlaji muislamu na wasiokuwa waislamu uhakika wa chakula tokea kilipoanzishwa hadi kuuzwa kuwa kimepitia njia inayotakiwa kwa misingi ya dini ya kiislamu.

"Katika kitabu cha Qur an kinatueleza kuwa tuchinje na tule vyakula vya halal lakini kwa sababu mbali mbali tumekuwa tukila chakula bila kujua kimeanzia wapi na kimepita katika njia gani" Kwa kutambua mchango wa dini yetu tumepata mafunzoambao ndio wamiliki wa nembo ya Halal baada ya mwaka mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa kile walichotuachia ili kueza kupata nembo hiyo itakayotusaidia kuuza bidhaa zetu katika nchi za Asia na nyenginezo, "alisema Lolila.

Ameongeza kuwa nchi nyingi za kiarabu hawali chakula mpaka waone nembo ya Halal ambapo wanaamini chakula hicho kimepita katika njia sashihi inayotakiwa kwa waumini wa kiislamu na wasiokuwa waislmu.

Huku akieleza kuwa Tanzania zipo bidhaa nyingi zitakazo weza kuingizia pato la Taifa kwa nchi hizo ikiwemo Malaysia endapo kama zitauzwa katika nchi za kimataifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halal Tanzania Certification (HTC) Muhsin Hussein amesema wamejifunza mengi kutoka kwa ugeni huo kutoka Malaysia na watayafanyia kazi mafunzo hayo yaliyowapa weledi wa kutambua bidhaa Halali kuanzia kwenye hatua za awali, na kuongeza kuwa wataitisha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari ili waweze kutoa elimu kwa Umma nao ujue kwa undani bidhaa Halal.

Mkurugenzi huyo amewatoa hofu a kwa kuwaeleza kuwa zile nembo za Serikali zinazotumika katika usimamizi wa bidhaa na chakula ikiwemo TBD na TFDA zitaendelea kuwepo ila nembo hiyo ya Halal itakuwepo ili kuweka Imani kwa waumini wa Dini ya Kiislamu waliokuwa na hofio ya kutumia bidhaa zisizo Halal, zinazokwenda kinyume na mafundisho ya Dini hiyo Tukufu.
Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani) juu ya Tanzania ijiandae kunufaika kibiashara na kukuza uchumi wa Taifa na mtanzania mmoja mmoja ifikapo mwakani leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mkurugenzi Msaidi JAKIM kutoka nchini Malaysia Mohd Amri Bin Abdullah.
Mkurugenzi Msaidi wa kampuni ya JAKIM kutoka nchini Malaysia,Mohd Amri Bin Abdullah akizungumza na waandi wa habari (hawapo pichani) juu kuzingatia viwango maalum vilivyowekwa na kampuni ya JAKIM nembo ya halali leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila Mkurugenzi wa Halal Tanzania Certification (HTC),Muhsin Hussein akifafanua jamb leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...