THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TANZANIA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA LA MCHEZO WA KABBADI NCHINI INDIA.

Timu ya taifa ya michezo ya Kabbadi nchini tanzania inatarajiwa kushiriki kombe la dunia la michezo ya kabaddi yatakayoanza rasmi novemba mwaka huu katika jimbo la Punjab.
Hayo yamebainishwa na balozi wa India nchini Tanzania Mh. Sandeep Arya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam na kueleza kuwa mchezo huo utashirikisha jumla ya watu 34 kati yao ikiwa ni timu ya wanawake na timu ya wanaume pamoja na makocha wa nne.

"Tunafuraha kwa nchi ya tanzania kupata washiriki watakaoenda nchini india kushiriki kombe hilo la dunia la kabadi wanaume wakiwa kumi na tano na wanawake kumi na tatu wakiongozwa na makapteni wao.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi idara ya maendeleo ya michezo,Alex NKenyenge ameongeza kuwa serikali ya Tanzania itazidi kutoa ushirikiano na nchi hiyo hususani katika michezo ya jadi huku akizitaka timu hizo kufanya vizuri katika michuano hiyo ili kuipeperusha bendera ya Tanzania."Michezo isiishie hapa hasa hii ya jadi bali ipewe kipaumbele zaidi iweze kufika mbali na hvyo viongozi wasing'ang'anie michezo iliyozoeleka"aliongeza kaimu mkurugenzi.
Kabaddi ni mchezo maarufu katika jimbo la punjab na mikoa mingine ya india ambapo hii ni mara ya sita kufanyika kwa kombe la dunia la mchezo huo ambapo kwa mwaka huu timu 13 kutoka sehemu mbalimbali za dunia zitashiriki ambazo ni Tanzania,USA,England,Kenya,India,Mexico n.k.

Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya akizungumza na waandishi wa habar juu ya Mashindano hayo yatakayo fanyika nchini India mapema leo jijini Dar es salaam.
Kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habar kuhusiana na Michuano hiyo leo jijini.

Timu ya Wachezaji wa Mchezo wa Kabaddi wakiwa katika Picha ya pamoja na Balozi wa India Nchini Bw Sandeep Arya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Mkenyenge leo jijini Dar.Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Kabaddi ndio mchezo gani?