Timu ya taifa ya michezo ya Kabbadi nchini tanzania inatarajiwa kushiriki kombe la dunia la michezo ya kabaddi yatakayoanza rasmi novemba mwaka huu katika jimbo la Punjab.
Hayo yamebainishwa na balozi wa India nchini Tanzania Mh. Sandeep Arya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam na kueleza kuwa mchezo huo utashirikisha jumla ya watu 34 kati yao ikiwa ni timu ya wanawake na timu ya wanaume pamoja na makocha wa nne.

"Tunafuraha kwa nchi ya tanzania kupata washiriki watakaoenda nchini india kushiriki kombe hilo la dunia la kabadi wanaume wakiwa kumi na tano na wanawake kumi na tatu wakiongozwa na makapteni wao.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi idara ya maendeleo ya michezo,Alex NKenyenge ameongeza kuwa serikali ya Tanzania itazidi kutoa ushirikiano na nchi hiyo hususani katika michezo ya jadi huku akizitaka timu hizo kufanya vizuri katika michuano hiyo ili kuipeperusha bendera ya Tanzania."Michezo isiishie hapa hasa hii ya jadi bali ipewe kipaumbele zaidi iweze kufika mbali na hvyo viongozi wasing'ang'anie michezo iliyozoeleka"aliongeza kaimu mkurugenzi.
Kabaddi ni mchezo maarufu katika jimbo la punjab na mikoa mingine ya india ambapo hii ni mara ya sita kufanyika kwa kombe la dunia la mchezo huo ambapo kwa mwaka huu timu 13 kutoka sehemu mbalimbali za dunia zitashiriki ambazo ni Tanzania,USA,England,Kenya,India,Mexico n.k.

Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya akizungumza na waandishi wa habar juu ya Mashindano hayo yatakayo fanyika nchini India mapema leo jijini Dar es salaam.
Kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habar kuhusiana na Michuano hiyo leo jijini.

Timu ya Wachezaji wa Mchezo wa Kabaddi wakiwa katika Picha ya pamoja na Balozi wa India Nchini Bw Sandeep Arya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Mkenyenge leo jijini Dar.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...