Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi, Dk. Othmani Kiloloma akifungua
rasmi sherehe za kuadhimisha siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo
wazi Duniani,ambapo alisema wanakazi kubwa ya kutoa matibabu kwa watoto
wenye matatizo ya mtindio wa ubongo na mifupa na mpaka sasa watoto
takribani 202 wameshafanyiwa upasuaji na zoezi linaendelea Nchi nzima.
Mwenyekiti
wa chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
Bw. Hakim ambaye nae mtoto wake anamatatizo kama hayo akielezea kuwa
kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa kuwa watu wengi wanahusisha tatizo hilo
na imani potofu, aliongeza kuwa watoto waliofanyiwa upasuaji mkoa wa
Mbeya ni 18, Morogoro 12, Mwanza 50, na Izazi 14. na wamefanikiwa kuokoa
Maisha ya watoto 185 katika mikoa 16 Tanzania.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao wenye vichwa vikubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...