THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TANZANIA YAIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA AFCON KWA VYUO VIKUU BEIJING CHINA

Timu ya Tanzania iliyochukua kombe baada ya kuitoa timu ya Ghana kwa Mikwaju ya Penalti katika mashindano ya mpira wa miguu kwa wanachuo wote wa Afrika wanaosoma Beijing Nchini China, yaliyomalizika hivi karibuni wakishangilia ushindi wao huo wakiwa na kombe lao.
Baadhi ya wanafunzi hao wakiwa na Bendera ya Taifa pamoja Kombe lao.


Kuna Maoni 3 mpaka sasa.

 1. HK Anasema:

  Huwa nakerekwa sana sana kila nnapoiona BENDERA yetu ya TAIFA inapopeperushwa hali ya kuwa imekamatwa au kushikiliwa 'kichwa chini miguu juu'. Hili nikimaanisha mpangilio wa rangi zake na inavyostahili kushikwa/kukamatwa. Ukiiangalia hiyo picha hapo imekamatwa ndivyo sivyo, si bora hata wangeangalia hata hiyo 'logo' iliyopo katika hizo T-Shirt zao, then wakaikamata kama inavyostahili. Nadhani ipo haja ya kuelimishana juu ya hili jambo, japokuwa litaonekana ni la kipuuzi, lakini lina umuhimu wake ikiwa ni kama mojawapo ya alama kuu ya utambulisho wa Taifa letu. Maana si mara moja wala mbili kuliona jambo hili. Ila nisiwe mchoyo wa fadhila, nawapongeza sana kwa kuibuka kidedea katika mashindano hayo na kuweza kuipeperusha bendera yetu.

 2. Anonymous Anasema:

  Hawa vijana wanaibeba baendera ya taifa juu chini?
  Waangalie kwenye tisheti zao walizovaa ilivyokaa kama hawajawahi kufundishwa au kuona sehemu nyingine.

 3. Anonymous Anasema:

  Pengine utafsiri wa rangi nao unawachanganya wengi kati ya blue na green. wakidhani blue ni maji yatokayo juu angani (mvua) badala ya mito na maziwa mengi tuliyojaliwa Tanzania na kijani ikiwa ni mimea/nyasi kama hizo walizokanyaga hapo ikimaanisha ambayo iko chini.