Timu ya Tanzania iliyochukua kombe baada ya kuitoa timu ya Ghana kwa Mikwaju ya Penalti katika mashindano ya mpira wa miguu kwa wanachuo wote wa Afrika wanaosoma Beijing Nchini China, yaliyomalizika hivi karibuni wakishangilia ushindi wao huo wakiwa na kombe lao.
Baadhi ya wanafunzi hao wakiwa na Bendera ya Taifa pamoja Kombe lao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Huwa nakerekwa sana sana kila nnapoiona BENDERA yetu ya TAIFA inapopeperushwa hali ya kuwa imekamatwa au kushikiliwa 'kichwa chini miguu juu'. Hili nikimaanisha mpangilio wa rangi zake na inavyostahili kushikwa/kukamatwa. Ukiiangalia hiyo picha hapo imekamatwa ndivyo sivyo, si bora hata wangeangalia hata hiyo 'logo' iliyopo katika hizo T-Shirt zao, then wakaikamata kama inavyostahili. Nadhani ipo haja ya kuelimishana juu ya hili jambo, japokuwa litaonekana ni la kipuuzi, lakini lina umuhimu wake ikiwa ni kama mojawapo ya alama kuu ya utambulisho wa Taifa letu. Maana si mara moja wala mbili kuliona jambo hili. Ila nisiwe mchoyo wa fadhila, nawapongeza sana kwa kuibuka kidedea katika mashindano hayo na kuweza kuipeperusha bendera yetu.

    ReplyDelete
  2. Hawa vijana wanaibeba baendera ya taifa juu chini?
    Waangalie kwenye tisheti zao walizovaa ilivyokaa kama hawajawahi kufundishwa au kuona sehemu nyingine.

    ReplyDelete
  3. Pengine utafsiri wa rangi nao unawachanganya wengi kati ya blue na green. wakidhani blue ni maji yatokayo juu angani (mvua) badala ya mito na maziwa mengi tuliyojaliwa Tanzania na kijani ikiwa ni mimea/nyasi kama hizo walizokanyaga hapo ikimaanisha ambayo iko chini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...