Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF –
umehitimisha mkutano wa wadau wa Maendeleo ambao wamepitia utekelezaji wa
shughuli za Mpango wa Kunusuru kaya maskini unaotekelezwa nchini kwa lengo la kuona utekelezaji wake katika
kipindi cha miezi sita iliyopita.
Licha ya kuwa na mkutano , wadau hao wa
maendeleo, maafisa kutoka baadhi ya wizara, taasisi za serikali na mashirika
yasiyokuwa ya kiserikali na watumishi wa
TASAF walipata fursa ya kutembelea wilaya za Mbarali, Muheza,Chato,Mkulama na
Pemba na kukutana na walengwa wa Mpango huo na kuona namna wanavyonufaika na
ruzuku ya fedha inayotolewa kwa kaya maskini.
Majumuisho ya mkutano huo yameonyesha
kuwa kuna mafanikio makubwa katika
utekelezaji wa shughuli za Mpango ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku kwa walengwa
kwa wakati, kuhamasisha walengwa kubuni miradi ya kujiongezea kipato na
kushirikisha jamii katika utekelezaji wa shughuli za Mpango.
Aidha imeelezwa kuwa kumekuwa na
mafanikio makubwa katika mahudhurio ya wanafunzi wanaotoka katika kaya maskini
na kuongezeka kwa mahudhurio ya watoto katika kupata huduma za kliniki mambo
ambayo ni miongoni mwa masharti kwa walengwa kupara moja ya ruzuku zinazotolewa
na Mpango wa Kunusuru kaya maskini.
Akizungumza mwishoni mwa mapitio hayo
ambayo hufanyika kila baada ya miezi sita, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana
Ladislaus Mwamanga ametaka jitihada zaidi ziendelee kuchukuliwa na wafanyakazi
wa TASAF na wadau wengine wanaotoa huduma kwa kaya maskini ili walengwa waweze
kunufaika na huduma za mpango.
Kwa
upande wake Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bwana Abdulahi
Muderis amesema mafanikio yaliyoanza kuonekana katika utekelezaji wa Mpango wa
Kunusuru kaya maskini ni kielelezo thabiti kinachoonyesha kuwa serikali ya
Tanzania imo katika jitihada kubwa za
kupambana na umaskini .
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga(aliyeshika kipaza sauti) akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wakifuatilia taarifa utekelezaji wa shughuli za Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wakifuatilia taarifa utekelezaji wa shughuli za Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
Baadhi ya watumishi wa TASAF wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo wakisikiliza taarifa za utekelezaji wa Mpango huo kwenye mkutano wa kupitia utekelezaji wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...