Wadau wa Maendeleo wanaoshirikiana na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini –PSSN- wameanza mkutano jijini Dar es salaam kupitia mafanikio ya utekelezaji wa Mpango huo.

Akifungua Mkutano huo wa siku moja, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo amesema Serikali inathamini na kutambua mchango wa wadau hao wa maendeleo katika kusaidia jitihada za kutokomeza umaskini miongoni mwa wananchi.

Bwana Ilomo amesema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia TASAF umekuwa wa mafanikio ya kuridhisha ambapo Zaidi ya kaya maskini Milioni Moja zimetambuliwa na kuorodheshwa kwenye Mpango huo nchini kote.

Aidha Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Rais amebainisha kuwa kwa kutambua umuhimu wa Mpango huo serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wake ili malengo yake yaweze kupatikana kwa haraka na kuwanufaisha walengwa na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Bwana Ilomo amezungumzia hatua zilizoanza kuchukuliwa dhidi ya watu waliopenyezwa kwenye Mpango bila kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuziondoa takribani kaya 30,000 zilizokuwa zimeandikishwa kinyume cha kanuni za Mpango.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema Mfuko huo umefanikiwa kulipa walengwa wa Mpango kwa awamu 17 nchini kote ambako katika maeneo mengi ya Mpango tayari mafanikio yameanza kuonekana ikiwemo walengwa kuboresha maisha,kusomesha watoto na hata kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi kwa lengo la kujiongezea kipato.

Wadau hao wa Maendeleo kesho watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali nchini na kukutana na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili kuona namna wanavyonufaika na ruzuku itolewayo na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF. 

Zifuatazo ni picha za tukio la ufunguzi wa mkutano wa TASAF na wadau wa Maendeleo uliofunguliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo akifungua mkutano wa wadau wa maendeleo ulioandaliwa na TASAF. 
    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo akizungumza na wadau wa Maendeleo Ikulu jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wadau wa maendeleo na watendaji wa TASAF wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa wadau awa maendeleo jijini Dar es salaam iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo( hayupo pichani). 
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akitoa maelezo kwenye mkutano wa wadau wa maendeleo jijiji Dar es salaam . 
 Wadau wa maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na katibu mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo baada ya ufunguzi wa Mkutano wenye lengo la kutathmini utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini .
 Wadau wa maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na katibu mkuu Ofisi ya Rais Bwana Peter Ilomo baada ya ufunguzi wa Mkutano wenye lengo la kutathmini utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...