Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
linapenda kutoa tahadhari kwa timu tano za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(VPL) juu ya kuwatumia wachezaji ambao imewasajili, lakini imebainika mbele ya
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwamba wana matatizo kwenye usajili wao.
Majimaji ya Songea
Mchezaji anayefahamika kwa majina ya George Mpole ambaye pia
amebainika kuwa ndiye Gerald Mpole wa Majimaji ya Songea amefungiwa kucheza
soka kwa mwaka kwa kosa la kubadili jina akiwa na lengo la kufanya udanganyifu
kwenye usajili. Majimaji imeagizwa kutomtumia mchezaji huyo kutoka Kimondo FC.
Mwadui FC ya Shinyanga
Mchezaji William Lucian aliyesajiliwa na Mwadui ya Shinyanga
kutoka Ndanda ya Mtwara, naye amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kusajili
Mwadui FC ilihali akiwa hajamaliza mkataba na Ndanda. Mwadui isimtumie mchezaji
huyo.
Mbeya City ya Mbeya
Mchezaji Saidi Mkopi, pia amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la
kujisali timu mbili. Imebainika kuwa akiwa bado na mkataba na Tanzania Prisons
ya Mbeya hivyo Mbeya City isi1mtumie mchezaji huyo.
African Lyon ya Dar es Salaam
Mchezaji Rehani Kibingu aliyesajiliwa na African Lyon ya Dar es
Salaam, amesimamishwa kuchezea timu hiyo mpaka uongozi wa African Lyon
kumalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam kabla ya Agosti 27, 2016. African
Lyon isimtumie mchezaji huyo kwa sasa.
Mbao FC ya Mwanza
Mchezaji Emmanuel Kichiba
aliyesajiliwa Mbao FC, naye amesimamishwa mpaka Mbao watakapomalizana na
Ashanti United ya Dar es Salaam, kabla ya Agosti 27, 2016. Mbao FC isimtumie
mchezaji huyo kwa sasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...