Ofisa wa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini(TFF), Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MWAMUZI Ahmed Seif amefungiwa kuchezesha mpira kwa miezi sita baada ya kutoa penati iliyokuwa sio sahihi pamoja na kupata alama chache ambazo haziruhusu kuchezesha ligi kuu katika mchezo baina ya African Lyon na Mbao uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF,kupitia kwa Ofisa habari wake Alfred Lucas amesema kuwa  klabu ya Simba imepigwa faini ya milioni tano
baada ya mashabiki wake kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa mali za serikali na kutakiwa kulipa gharama za uharibifu huo kupitia kanuni ya 42(3) na 24(7) huku Msemaji wa timu hiyo Haji Manara akipigwa faini ya laki mbili kwa kosa la kuingia ndani ya Uwanja pasi na kuwa kiongozi wa benchi la Ufundi kulingana na kanuni ya 14(10).


Simba wamepewa adhabu hiyo ya faini iliyotokea katika mchezo wao dhidi ha Yanga uliofanyika Oktoba 1, uliochezeshwa na Mwamuzi Martin Saanya ambaye mpaka muda huu kamati ya bodi ya ligi inaendelea na uchunguzi wa mchezo mzima ili kutoa maamuzi huku wakiifuta kadi nyekundu aliyepewa Nahodha Jonas Mkude kupitia kanuni ya 9(8).

Klabu ya Azam imepigwa faini ya milioni tatu kwa kosa la kuvaa nembo ya mdhamini katika mikono yote ikiwa ni kanuni ya 13(6), JKT Ruvu imepigwa faini ya milioni tano kutokana na kushambuliwa kwa msimamizi wa kituo na ofisa wa bodi ya ligi na mshabiki wa timu hiyo na tayari wamemfungia kwa kipindi cha mwaka mmoja na kama wataendelea na kitendo hicho basi wataufungia kutumika kwa Uwanja huo.

Wakati huo, kamisaa wa mchezo namba 5 na 7,  David Lugenge na Godbless Kimaro wamepewa onyo na bodi ya ligi baada ya kuandika ripoti isiyojitosheleza kwenye michezo hiyo.                         

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...