TIB Corporate bank imefanya Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja wake yaliyoambatana na ufunguzi rasmi wa ofisi mpya za benki hiyo tawi la Arusha katika Jengo PPF Plaza.

Akizungumza jijini Arusha wakati hafla hiy, Mkurugenzi Mtendaji TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege alisema kuwa wao kama benki mejipanga kuisaidia serikali katika kufanikisha malengo yake ya kujenga viwanda na kulifikisha taifa katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“TIB kama benki tumejipanga kuisaidia serikali katika kufanikisha malengo yake ya kujenga viwanda na kulifikisha taifa katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, kwani Hakuna benki hapa Tanzania unayoweza kuifananisha na TIB. Tuna TIB Development Bank taasisi ya fedha inayotoa mikopo ya muda mrefu ya miradi mikubwa ya maendeleo,TIB Corporate Bank tunatoa huduma za mikopon ya uendeshaji wa biashara na tuna Benki ya Rasilimali inayotoa huduma za ushauri wa uwezekaji na uwakala wa mitaji na hisa.” Alisema Nyanbundege.
Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali (mstaafu) Mirisho Sarakikya akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege (kulia) katika hafla ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwenye ofisi mpya za benki hiyo jijini Arusha.

“Tunawahakikishia wateja wetu kwamba tutaendelea kuboresha huduma zetu na bidhaa zetu ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya kibiashara na TIB taasisi pekee ya kifedha unayoweza kupata huduma zote za kifedha.” Alimalizia.

Mmoja wa wateja wa benki hiyo, Dk. Philemon Mollel wa Monaban Trading and Farming Company Limited aliipongeza beki hiyo kwa kuwapa kipaumbele wateja wake wa kanda ya kaskazini, hasa namna inavyowarahisishia miamala ya fedha na ufanisi wa bishara zao.
Mkurugenzi Mtendaji TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege (katikati) akibadilishana mawazo na mmoja wa wateja wa benki hiyo (kushoto) wakiwa pamoja Meneja TIB Development Bank kanda ya Kaskazini, Heri Kalungwana.

Ili kuwaongezea wigo wa kibiashara wateja wake, benki hiyo hivi karibuni iliingia mkataba wa ubia na Benki ya Posta Tanzania (TPB) unaoiwezesha benki hiyo kutoa huduma zake kupitia matawi makubwa na madogo ya benki ya Posta yaliyopo kote nchini.

Hivi karibuni pia benki hiyo ilifungua tawi lake kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Dar es Salaam ikilenga kusogeza huduma zake kwa ubora zaidi katika bandari hiyo.

TIB Corporate Bank Limited ni benki ya kibiashara inayo milikiwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa asilimia miamoja. Benki ni sehemu ya benki ya TIB Development Bank.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...