Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii.
MAKAMPUNI makubwa ya jimbo la Henan nchini China wametembelea Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (TIC), Clifford Tandari, amesema kuwa watu wenye makampuni  kutoka jumbi hilo wamekuja kuangalia uwekezaji katika maeneo viwanda, madini, pamoja tehama.

Amesema kuwa baada ya kutoka TIC watakwenda sehemu nyingine za serikali kuweza kupata maelezo zaidi ya juu ya uwekezaji.

Tandari amesema wamejipanga kufanya uwekezaji  nchini na kuweza kufikia uchumi wa viwanda. Aidha amesema kuwa katika kufanya uwekezaji TIC ndio imepewa dhamana hiyo .
 Picha ya pamoja ya kaimu Mkurugenzi Mtendaji akiwa watu wenye makampuni katika jimbo la henani leo jijni Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa bodi, Katibu wa Henan Investment Group co.Ltd. Lianchang Zhu akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara yao ya kuja kuangalia mazingira ya uwekezaji nchini.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Clifford Tandari (Kulia)akizungumza na waandishi wa habari juu makapuni ya jimbo la Henan walivyodhamiria kuwekeza nchini leo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...