Timu za soka za Simba na Yanga za Jijini Dar es Salaam zimezuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana kutoka na mashabiki wao kusababisha uharibifu wa miumbombimu ya Uwanja  wa Taifa yakiwemo mageti ya kuingilia Uwanjani na kung’oa viti kwa upande wa mashabiki wa Simba.
Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akikagua na kutembelea maeneo yalioathirika na uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba na Yanga katika mechi iliyochezwa Octoba Mosi 2016 katika Uwanja wa Taifa.
“Hii si mara ya kwanza kwa mashabiki kuvunja mageti na kung’oa viti na sisi kama Serikali tumeamua kuzuia vilabu hivi vya Simba na Yanga kutotumia Uwanja wa Taifa mpaka tuitavyoamua vinginevyo hapo baadae” Alisistiza Mhe. Nnauye.
Mhe. Nape Nnauye ameongeza kuwa wameendaa mfumo wa kutumia kamera Uwanjani ili kubaini makosa yatakayokuwa yanafanyika ili kuzuia vitendo vya kihualifu na uharibifu katika Viwanja vya michezo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa wamesikitishwa sana na uharibifu ulitokea katika mechi ya Simba na Yanga na kusababisha uharibifu wa viti na mageti ya kuingilia Uwanjani.
Ameongeza kuwa kwa tathimini iliyofanyika mageti manne yameng’olewa na mashabiki kwa upande wa Simba na Yanga na pia kwa upande wa ndani jumla ya viti 1781 vimeng’olewa katika upande wa mashabiki wa Simba.
“Mara nyingi tumekubaliana kutunza Uwanja huu kwa ajili ya matumizi ya watanzania wote na kama wasimamizi tunasikitika kwa kitendo hiki kilichotokea na tujue kuwa ni kodi za wananchi ndio zilitumika kujenga Uwanja huu na pia ndizo zitazotumika kukarabati Uwanja tuwe na tabia ya kupenda na kutunza vya kwetu.
Klabu za Simba na Yanga zimekuwa na ushindani mkubwa katika soka la Tanzania na kumekuwa kukitokea mambo mbalimbali pale timu hizo zinapokutana ikiwemo uharibifu wa miundombinu katika Viwanja na vurugu kwa mashabiki pale mmoja wao anapofungwa.

 Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Serikali kuzuia timu za Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akiwa amekaa akiangalia jinsi viti vilivyong’olewa katika Uwanaja wa Taifa na Serikali   kuchukua uamuzi wa kuzuia timu za Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa na kuzuia mapato ya mechi waliyocheza mpaka watakapolipa fidia  kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.

Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akitazama moja ya kiti kilichong’olewa jana katika mechi ya Simba na Yanga na Serikali kufikia  uamuzi wa kuzuia timu hizo kutumia Uwanja wa Taifa kutoka na uharibifu wa miundombinu uliotokea katika mechi yao iliyofanyika Oktoba Mosi 2016.

 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathimini iliyofanyika mara baada ya mechi wa jana kati ya Simba na Yanga na jumla ya mageti manne yamevunjwa na viti1781 vimeong’olewa katika Uwanja wa Taifa.
  Eneo liliong’olewa viti katika Uwanja wa Taifa katika mechi ya Simba na Yanga iliyofanyika Oktoba Mosi. 
Habari na Picha na Raymond Mushumbusi - MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. The football hooligan has arrived
    Tukio hili ni la kuhuzunisha sana, naona kama virusi vya magonjwa ya uhuni kwenye football nimewaambukiza ndugu zetu. Dawa yake ni adhabu za kutisha. Timu husika zipigwe faini ya kutisha, kila timu pia ipewe maagizo ya kuwa na marshalls wao wa kukontrol mashabiki wao. Football hooligans will ruin the good game,I know what they can do, I have seen them at work in Europe na Ukerewe.

    ReplyDelete
  2. Mimi nadhani ujinga umechangia kiasi kikubwa kwenye matukio hayo na nadhani hatua ya awali iliyochukuliwa ni bora lakini pia kama watapatikana watu binafsi ( wapumbavu) wakachukuliwa hatua kali zaidi lingepunguza kama si kumaliza upumbavu wa watu wasiopenda maendelea na wenye akili finyu kama hao, ulaya sio Afika (Tanzania)hawawezi kutuharibia kidogo kizuri tulichonacho.

    ReplyDelete
  3. Inasemekana football ilianza Uingereza, na uhuni wa football pia ulianza uingereza. Lakini angalia sasa kuna The Bad Blue Boys ambao wakikutana na Red Star Belgrade inakuwa ni kama vita vya dunia. Kuna Irriducibili ambayo hata wachezaji wa kimatumbi wanawaogopa,Na kuna jirani zetu kule Milwall, wanatisha, na wimbo wao""Hakuna atupendaye na hatujali (translated)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...