Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza kwenye  mkutano wa baraza la madiwani  juu ya kufanya kazi kwa masilahi ya wananchi na sio kupelekwa kama Kondo leo mkoani Pwani.
 Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Saum Ally Papen ajifafanua jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani leo  mkoani Pwani.
Sehemu ha madiwani. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, Mkuranga.
MBUNGE wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa baraza la madiwani wafanye kazi kwa masilahi ya wananchi na sio kupelekwa kama Kondoo.

Ulega ameyasema hayo leo katika baraza la Madiwani wa Mkuranga katika ulidhiaji wa Ekari 250 ambazo zitatimika katika miradi mbalimbali ya Halmashauri hiyo.

Amesema kuwa mchakato wa kupata ardhi hiyo ulianza muda mrefu hivyo ulipofikia ni pazuri kwa watendaji kijipanga.

Aidha amesema wananchi wanataka maendeleo na majukumu hayo ni madiwani ni kuwajibika pamoja na Wabunge."Mkuranga iko nyuma kimaendeleo hivyo kila kiongozi afanye kazi kwa ajili ya Mkuranga". Amesema Ulega.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid amesema ukusanyaji wa mapato uko chini hivyo kunahitaji nguvu katika ukusanyaji wa mapato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...