Mwenyekiti
wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Ndg Simai Mohammed Said
akitiliana saini ya Makubaliano ya kusaidia Tamasha la Sauti za Busara
Zanzibar na Balozi wa Ujerumani Tanzania Balozi Egon Kochanke, Ujerumani
imekubali kuchangia €5000 sawa na shilingi za Kitanzania milioni 12,hafla
hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Park Hyyat
Shangani Zanzibar leo. Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar hufanyika
kila mwaka katika mwezi wa Febuary na kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali
wanaotembelea Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said,
akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Balozi Egon
Kochanke, baada kumaliza kutiliana saini ya makubaliano ya kuchangia
Tamasha hilo kwa mwaka 2017, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa
Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar, leo mchana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...