Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo  katika ufunguzi mkutano wa wadau wa sekta Binafsi kujadili Tanzania ya Viwanda ya 2020 Tunayoitaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPST, Godfrey Sembeye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya maendeleo ya TPSF katika ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya viwanda wakiwa katika ufunguzi mkutano wa wadau wa sekta Binafsi kujadili Tanzania ya Viwanda ya 2020 Tunayoitaka jijini Dar es Salaam leo.

Na Yassir Adamu, Globu ya Jamii.
TANZANIA ni miongoni mwa nchi zinazongoza Afrika kwa kuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi ya miujiza.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam, Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte katika ufunguzi mkutano wa wadau wa sekta Binafsi kujadili Tanzania ya Viwanda ya 2020 Tunayoitaka, amesema ukuaji wa uchumi katika miongo miwili iliyopita huku pato la taifa lilikikua kwa wastani wa asilimia 7.0 kwa mwaka katika kipindi cha kuanzia 2007/2015 lakini lengo la kukua ni asilimia Nane hadi 10 ili kuweza kutokomeza umasikini uliokidhiri nchini.

Amesema katika kutekeleza na  kufanikisha lengo la kitaifa la kuongeza kipato cha mtanzania mmoja mmoja hadi kufikia Dola za Kimarekani Tatu (3,000) ifikapo 2025.

Shamte amesema viwanda vina jukumu muhimu katika kusaidia Tanzania kuinua viwango vya ukuaji wa uchumi katika upatikakanaji wa ajira na kuboresha maisha ya watu .

Aidha amesema katika fursa ya viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo ambapo mazao hayo yanauzwa asilimia kubwa kama mali ghafi.

Shamte amesema kuuzwa kwa  mazao ya kilimo kama mali ghafi inachangia kudororesha kukua kwa sekta ya kilimo ambayo iinakua kwa wastani wa asilimia 4.2 tu na kufanya umasikini kuendelea kuwepo kwa kiwango cha juu na kufanya sekta hiyo kuwa na ajira asilimia 67 ya watanzania kwa sasa.

Amesema sekta binafsi imepewa nafasi kubwa kuchangia maendeleo ya nchi yetu kutokana Rais Dk.John Pombe Magufuli kuonyesha nia kufanya majadiliano ya masuala sekta binafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...