THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UCHUMI WA VIWANDA WAHITAJI ELIMU YA UFUNDI IMARA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo (kulia) akimkabidhi  nakala za jarida la   utekelzaji wa shughuli za baraza la wafanyakazi Kaimu Katibu  Mtendaji wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) , Dk Adolf Rutayuga  kwenye hafla ya  uzinduzi wa baraza hilo la kwanza la  wafanyakazi  wa NACTE jijini Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2016. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NACTE, Mhandisi, Stephen Mlote.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo (kulia) akizindua  baraza la kwanza la wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jijini Dar es Salaam jana. na kushoto ni Mwenyekiti nwa Bodi ya NACTE, Mhandisi Stephen Mlote.
Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wakimsikiliza kwa makini Naibu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo  ambaye alizindua bara za kwanza la wafanyakazi  wa NACTE jijini Dar es Salaam leo Oktoba 4, 2016.

Na Mwandishi Wetu
Taasisi  ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi  (NACTE) ina dhamana kubwa ya hatma ya Elimu ya Ufundi  nchini Tanzania, jambo linafanya  elimu ya  Ufundi kuwa ya umuhimu  hususan katika kipindi hiki ambacho agenda kuu ya Taifa ni kujenga Uchumi wa Viwanda  kwakujenga  elimu ya ufundi imara.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu Sayansi na Teknlolojia, Dk Leonard Akwilapo wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa NACTE jijini Dar es Salaam leo Oktoba 4,2014.
Dk Akwilapo alisema kuwa  agenda hiyo inabidi ichukuliwe na Baraza hili kama kigezo cha kupima utendaji wa kazi wa NACTE.