Na Yusuph Kileo
Takwimu za uhalifu mtandao zimeendelea kukua huku wana usalama mtandao wakiendelea kutafuta suluhu ya kudumu dhidi ya uhalifu mtandao maeneo mengi duniani. Hivi sasa tumefikia wakati wa kila tunavyotumia ku unganishwa kwenye mtandao (Internet of Things – IoT) ambapo Televisheni, Friji , Majiko, Magari na kadhalika vimekua vikiunganishwa mtandaoni ili kurahisisha maisha ya watumiaji. 
Hali hii imepelekea wimbi kubwa la uhalifu mtandao kuendelea kukua na imetabiriwa kadri muda unavyoendelea tishio la uhalifu mtandao litakua kubwa zaidi – Kuliangalia hili Mkutano wa wana TEHAMA wa Nchi za Afrika (AfICTA) wa mwaka huu 2016 ambao uliofanyika jijini Windhoek Nchini Namibia ulipata kujadili mengi kuhusiana na hili ambapo pande mbili za faida na changamoto ziliangaziwa kwa karibu. 
Binafsi, Nilipata kushiriki kuongoza mijadala miwili ambapo tuliangazia changamoto za ukuaji wa uhalifu mtandao kutokana na wimbi wa vitu vingi kuendelea kuunganishwa mtandaoni na pia kujadili mapendekezo ya mambo ya msingi ya kuzingatia ili kubaki salama pamoja na mambo ya msingi kwa wadhibiti wa uhalifu mtandao wanayopaswa kuzingatia ili kuweza kudhibiti hali hii. Kusoma zaidi BOFYA HAPA. 
 Usiku wa Jana jijini #Windhoek, Namibia, Mdau mkuu wa Usalama wa Mtandao wa Tanzania Yusuph Kileo amepokea  Tunzo yake ya Kwanza ya kimataifa Kubwa  katika kutambua mchango wake mkubwa Barani katika swala la Usalama mtandao! Yusupha hakika amemefurahi sana! Kwani jina lake  litaingia katika majina yanayotegemewa kujadiliwa ili kuingia katika bodi ya wana TEHAMA wa Nchi za Afrika! Hatua muhimu kwake na Tanzania.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...