THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

ULEGA AZINDUA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA MSINGI MITAWA ,WILAYANI MKURANGA

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, amezindua ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi ya Mitawa,mwishoni mwa wiki,wilayani Mkuranga,Pwani,Ujenzi wa madara hayo unafuatiwa kutokana na shule ya hiyo kuwa na upungufu wa madarasa na kupelekea wanafunzi kusomea katika jengo la kupanga.

Akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Mitawa, Ulega amesema karne hii wanafunzi kusoma katika jengo la kupanga imepitwa na wakati, hivyo ni lazima wazazi wajitoe kujenga shule na serikali itatia mkono wake baada ya kuona njia ya kufanikisha jambo hilo.

Amesema suala linaloweza kufanya Taifa kuwa na maendeleo ni pamoja na kuwa wataalam ambapo lazima watoto waandaliwe katika mazingira ya shule na bila kufanya hivyo hakuna maendeleo hayo.Ulega amesema kama mbunge anawajibu wa kusimamia suala la elimu, kwa wananchi wa Mkuranga wanapata maendeleo ya elimu kwa kuwa na shule pamoja na walimu wa kutosha.

Katika ujenzi wa shule hiyo Mbunge amechangia zaidi ya milioni mbili na kuahidi kuendelea kutoa mchango mpaka pale shule itakapokamilika.Aidha amesema kufikia Januari shule hiyo imekamilika na wanafunzi waweze kuanza kusoma katika madarasa hayo na kuachana na kupanga jengo ambalo linatumika kwa sasa.
  Mbunge wa mkuranga akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya  ujenzi wa darasa la shule ya msingi Mitawa pamoja na shughuli ya ufyatuaji matofali Mbunge huyo pia alishiriki upandaji miti na kuzungumza na wananchi,leo mkoani Pwani.
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Mitawa, Mkuranga juu ya maendeleo yaliyofikia katika Shule ya Msingi  Mitawa, leo.
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega wapili (kutoka kushoto)  akishiriki mazoezi na vijana wa Mkuranga leo ikiwa ni sehemu ya kuwajenga vijana kuwa imara katika michezo.
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizindua vyumba viwili vya madarasa viliyojengwa na wananchi kwa kushirikiana na ofisi ya  mbunge leo.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
 Mbunge wa mkuranga ashiriki ujenzi wa darasa la shule ya msingi Mitawa pamoja na shughuli ya ufyatuaji matofali Mbunge huyo pia alishiriki upandaji miti na kuzungumza na wananchi,leo mkoani Pwani.