Serikali imesema iko makini na itahakikisha kuwa nchi inakuwa na usalama wa kutosha wa chakula kwa kuongeza uzalishaji ili kuendana na idadi ya watu inayoongezeka.

Akiongea wakati wa mkutano wa wadau wa mbolea toka ndani na nje ya nchi uliofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, alisema pamoja na juhudi nyingine zinazofanyika, wanasayansi na watafiti wametakiwa kuhakikisha kuwa taarifa zinazopatikana kuhusu udongo zinatumika ipasavyo ili kutoa suluhisho linalotakiwa pale inapohitajika.

“Taarifa hizi zitasaidia kufahamu maeneo yenye rutuba kidogo, sumu na hivyo kupata majibu yanayotakiwa,” alisema.

Katibu Mkuu huyo alitaja moja ya mikakati ya kuongeza uzalishaji wa mazao kama ushirikiano kati ya serikali na taasisi inayojulikana kama Africa Soil Information Services (AfSIS) na kitengo kipya katika Wizara hiyo kinachoitwa Tanzania Soil Information Services (TanSIS) ambapo ardhi yote nchini itapimwa na kufanyiwa tathmini ili kujua ubora wake.

Alisema mkakati huo utasaidia kujua mahitaji ya maeneo husika na kuwasiliana na kampuni za kuzalisha mbolea.Aliiomba taasisi ya African Fertilizer and Agribusiness Partnership (AFAP) na wadau wengine kushirikiana na TanSIS ili kuhakikisha kuwa panakuwa na matumizi bora ya mbolea nchini.
 
Takwimu zinaonyesha kuwa matumizi ya mbolea bado ni madogo sana katika eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
 
Mwaka 2005 hadi 2010, wastani wa matumizi ya mbolea Afrika ilikuwa metriki tani milioni 3.2 kwa mwaka ikilinganishwa na metriki tani milioni 74.1 (Asia), 19.5 (Marekani) and 13.0 (Ulaya).

Kwa mujibu wa Dr. Turuka, matumizi haya madogo ya mbolea yanatakiwa kuboreshwa haraka kama kweli Afrika inataka kuzalisha chakula cha kutosha watu wake.“Maboresho katika sekta ya kilimo hayana budi kuimarishwa sasa kuliko kipindi chochote kutokana na idadi ya watu inayoongezeka na mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema.

Wakati wa uhuru mwaka 1961, Tanzania ilikuwa na watu takribani milioni 9.  Idadi hiyo imeongezeka kufikia karibu watu milioni 50 mwaka 2016 katika eneo la ukubwa wa ardhi lile lile la kilometa za mraba 945,000,000.

Wataalamu wanakubaliana kwamba matumizi ya mbolea yenye virutubisho vingi kama njia ya kuongeza tija na kuboresha mazingira katika uendeshaji wa kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...