THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UTT-AMIS YAZINDUA HUDUMA MPYA YA USIMAMIZI WA MALI

MFUKO  wa Uwekezaji wa Pamoja  (UTT-AMIS)  umesema  kutokana na utafiti walioufanya  kwa muda wa miaka 10, unaonyesha Watanzania walio wengi  hawana  uelewa  wa   kuwekeza fedha zao  kwenye hati fungani (bond).
 Kauli hiyo  imetolewa  jijini Dar es Salaam na  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa  UTT,  Daudi Mmbaga , alisema  watu wengi wanakuwa na fedha nyingi lakini hawajui  jinsi ya kuwekeza  fedha zao.
 Alisema  kutokana na  changamoto iliyopo kwa Watanzania  ya kutokuwa na uelewa wa  jinsi ya kuwekeza , wameamua kuanzisha huduma ya  Usimamizi wa Mali  itakayomsaidia mwananchi  jinsi ya kuweza kuwekeza fedha zake na kutengeneza faida.
“ Watu wengi   wanakuwa  na fedha nyingi  lakini  zimelala tu, na wengine  wamewekeza   kwenye maeneo yasiyowapa faida  ndio maana tuamua kuanzisha huduma itakayowasaidia  kuwekeza  fedha yao  inayoitwa  Usimamizi wa Mali,” alisema.
 Aidha, alisema huduma hiyo  kwa sasa imeshaanza kutumika na  mwelekeo   ni mzuri  kutokana na  watu wengi  kupenda kuwekeza fedha zao, ambapo kiwango cha kuanzia ni sh. Milioni  tano.
 Mmbaga  alisema   kiwango  cha elimu  nchini  kikijikita vizuri kitasababisha  kuwepo  na soko la uhakika   na kusababisha  kuwepo na maendeleo   ya kiuchumi.
 Hata hivyo  aliwashauri wananchi kujitahidi kuwekeza katika mifuko  ya uwekezaji  kwa kuwa  kutasaidia  kuwa na imani na fedha zao.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Uwezeshaji (UTT-AMIS), Daud Mbaga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu huduma yao mpya ya usimamizi wa mali. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Issa Wahichinenda.