Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID), imekutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini pamoja na wadau katika kuboresha miundombinu, semina iliyofanyika mapema jana Oktoba 19 katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Semina hiyo iliyofunguliwa na mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo, Bw. Juston Lyamuya aliipongeza UTT-PID kwa namna ilivyoweza kubobresha miundombinu pamoja na shughuli za kimaendeleo hususani katika upatikanaji wa viwanja na hati kwa wananchi kwenye miradi yake mbalimbali hapa nchini.

“Sote kwa pamoja tunaipongeza UTT-PID, kwa namna inavyoendesha shughuli zake hasa katika sehemu mbalimbali za Halmashauri, Miji na Manispaa kwani zimeboresha miundombinu na hta wananchi kufaidika na miradi hii ambayo ipo kwa uwazi sambamba na kuendeshwa kisasa” amesema Mgeni rasmi huyo.

Katika semina hiyo, mada mbalimbali zimewasilishwa na wadau ikiwemo miradi ya upamaji ardhi, miundombinu, ujenzi na fursa zilizopo katika maeneo ya Majiji, Miji na Halmashauri hapa nchini.Aidha, Manispaa ya Lindi ilipongezwa kwa namna ya kipekee kufikia malengo katika miradi yake na UTT-PID Kwani ubia wao huo umekuwa wa mafanikio makubwa.

Naye Mkurugezi wa Manispaa ya Lindi Jomary Satura wakati wa kuwasilisha mada katika semina hiyo juu ya fursa za uwekezaji zinazopatikana katika manispaa hiyo, amewaomba wananchi na wadau kujitokeza kwa wingi Manispaa ya Lindi ilikunufaika zaidi na fursa zilizopo.Mgeni rasmi katika semina hiyo, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo, Bw. Juston Lyamuya akifungua rasmi semina hiyo ya Wahariri wa Vyombo vya Habari pamoja na Wadau wa UTT-PID katika semina ya ushirikishaji wa wadau katika kuboresha miundombinu, uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam jana Oktoba 19.2016.
Mkurugezi mkuu wa UTT-PID Gration Kamugisha akifunga semina hiyo kwa Wahariri wa vyombo vya habari (Hawapo pichani) na wadau wa mbalimbali katika semina ya ushirikishaji wa wadau katika kuboresha miundombinu, uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es salaam jana Oktoba 19.2016.
Mkurugezi wa Manispaa ya Lindi Jomary Satura akitoa semina kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana katika manispaa hiyo wakati wa mkutano wa jukwaa la wahariri lililoandaliwa na Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...