UMOJA wa Vjana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umelihimiza Jeshi la polisi nchini kutambua kuwa ujambazi, wizi wa kutumia silaha na uporaji bado ni tatizo linalohitaji kushughulikiwa kwa nguvu zote kama ambavyo nchi ilisimama na kutekeleza operesheni mbalimbali za ukombozi.

Pia, umesisitiza kuwa usalama wa raia na mali zao unahitaji kulindwa ili kuepusha vifo, hasara, unyang’anyi wa mali na vilema vya maisha kutokana na matukio yanayoweza kuwakumba wasio na hatia mijini na vijijini.Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alieleza hayo jana alipomtembelea kumjulia hali majeruhi Said Ally, Mabibo Hostel.

Saidi alijeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwa ni pamoja na kutobolewa macho katika tukio wizi wa kutumia silaha Buguruni mjini Dar es Salaam, Septemba mwaka huu.Shaka alisema tatizo la uhalifu, unyang’anyi, uporaji na ukwapuaji mali kwa kutumia nguvu na silaha, linahiaji kutazamwa kwa kina na upana unaostahili na vyombo vyenye dhamana vinavyosimamia usalama wa raia na mali zao.

Alisema kuna haja ya polisi kubuni mbinu mpya za kukabiliana na makundi ya wezi, waporaji na majambazi kabla hawajaleta madhara na hasara kama ilivyomtokea Said ambaye sasa ni amesababishiwa ulemavu wa kudumu wa kutoona.“Kila siku mbinu za uhalifu, ujambazi, wizi wa kutumia nguvu na silaha hubadilika, jukumu la kupambana na matukio hayo hatari ni la polisi kwa kushirikiana na raia wema, janga hili likiachwa wananchi wataishi kwa mashaka na hawatajituma kujiletea maendeleo,”alisema Shaka.

Alisema ikiwa wananchi wanajituma kwa bidii kutafuta fedha na kubuni miradi ya kiuchumi halafu majambazi na wanyang’anyi wanapora na kumfilisi aliyetafuta ndani ya saa chache, hilo linaweza kuwatia hofu mwananchi na wajasiriamali na kuwafanya washindwe kujituma kikamilifu jambo ambalo litakuwa na madhara makubwa katika kuzalisha mali na kukuza uchumi.

Akizungumza kwa masikitiko na huzuni kubwa , Shaka alisema tamaa ya kupata utajiri kwa njia haramu kwa mtu mmoja mmoja au kikundi, kumemsibaishia hasara ya maisha dhidi ya Said ambaye kwa sasa amekoseshwa uwezo wa kuendelea kupiginia maendeleo yake ya kiuchumi na taifa kwa ujumla.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...