Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Askari Mgambo walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mara baada ya kufunga maadhimisho ya miaka 52 ya JWT jana. 
 Askari Mgambo  na wanajeshi walioshiriki katika zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' katika kijiji cha Baatini Wilayani Bagamoyo mara baada ya kufunga maadhimisho ya miaka 52 ya JWT jana. 


Na: Frank Shija, MAELEZO
UZALENDO umewapatia ajira takribani vijana 70 baada ya Amiri Jeshi Mkuu,na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufurahishwa na namna ambavyo washiriki wa zoezi la Amphibia Landing walivyoonyesha umahiri wao.
Hayo yamebainika jana katika fukwe za kijiji cha Baatani, wilayani Bagamoyo, wakati wa hafla kufunga mazoezi hayo ambapo Mhe. Rais Magufuli alisema kuwa kutokana na alivyojionea mazoezi hayo na amearifiwa kuwa kati ya washiriki wa mazoezi hayo wamo mgambo 30 na JKT 40 aliagiza wote waingizwe kwenye orodha ya waajiriwa wapya wa JWTZ.
“Katibu Mkuu Kiongozi nakuagiza Kufanya utaratibu waku waingiza kwenye ajira hawa vijana 30 wa mgambo na 40 wa JKT kwani wameonyesha moyo wa uzalendo kwelikweli, tena ikiwezekana ata kesho waingie kwenye orodha ya waajiriwa wapya”. Alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange kuangalia namna ya kuwapa motishi wote walioshiriki kufanikisha zoezi hilo ili kuwaongezea morali ya kuwajibika.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa Majeshi kushirikia hususan katika eneo la unzanzishaji wa viwanda ili kutoa mchango wao katika hasma ya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
“Ni lazima sasa tujipange nataka Majeshi yetu muwekeze katika viwanda iwe kwa kuunganishwa nguvu pamoja ama mmoja mmoja naamini hatushindwi, leteni mpango Serikali itasaidia”. Alisema Rais Magufuli.
Alitolea mfano wa Jeshi la Magereza kuwa na kiwanda cha viatu katika Gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro, kushangaa kuona majeshi mengine yananunua viatu kutoka nje ya nchini. Aliwaagiza washirikiane katika kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa na viwanda.
Alisema kuwa Jeshi letu limekuwa na mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu yake ambayo aliyataja kuwa ni ulinzi wa mipaka ya nchi, kulinda katiba ya nchi, kufundisha wananchi masuala ya ulinzi wa Taifa, uokoaji na utoaji wa misaada katika maafa, kutoa elimu ya kujitegemea pamoja na ulinzi wa amani na ukumbozi.
Nakuongeza kuwa limeweza kulinda mipaka ya nchi, na kulinda amani iliyopo pamoja na kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kulinda amani katika baadhi ya maeneo ikiwemo Sudan Kusini na DRC Congo.
Septemba Mosi mwaka huu JWTZ walitimiza miaka 52 ya uhai wake,ambapo ilianza kuadhimsha miaka hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali kama vile usafi, huduma za upimaji wa Afya Bure na zoezi hili la Amphibia Landing ni muendelezo wa maadhimisho hayo.
Ambapo katika zoezi hilo vifaa kama Meli Vita, Vifaru vinavyo tembea nchi kavu na majini, milipuko pamoja na Ndege vita vilitumika. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pongezi za dhati na za pekee kwa Mh. Rais wetu John Pombe Joseph MAGUFULI kwa kuwafikiria katika suala la ajira kwenye JWTZ vijana hao 70 walioonyesha moyo wao wa uzalendo katika hafla hiyo. Hata wahenga walisema siku zote...mcheza kwao hutunzwa." Nadhani hilo litazidi kuwatia ari na kuwapa moyo hata vijana wengine wengi katika kujitolea na kujituma kwa dhati kwenye shughuli mbali mbali khususan katika kuleta maendeleo ya nchi yetu na ujenzi wa Taifa letu kwa jumla. Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  2. Naungana na mtoa pongezi hapo juu. Kwanza pongezi kwa Amirijeshi Mkuu, Mheshimiwa Rais JPM. Pili kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na viongozi wa Majeshi yote Nchini. Watanzania popote tuendapo duniani tunatembea vifua mbele kwa kujivunia amani yetu ambayo hao nilowataja ndio wanaoongoza. Pia Makamanda na wapiganaji wengine wote katika levels tofauti, HONGERENI SANA. Rais wetu ni mzalendo nambari 1. Hapa hakuna ubinafsi wala upendeleo. Vijana wameonesha uwezo na ari ya kuilinda nchi yao. Hongereni vijana wetu. Basi kutembea kwetu kifua mbele kutaendelea kwani nyie mmeamua kuilinda mipaka ya nchi na kushiriki katika ulinzi na usalam wa nchi. Yeyote atakayesoma makala hii na kumgusa, HONGERA SANA. Iwe wewe ni mzazi au ni kijana mwenyewe, HONGERA SANA Na enedelea na moyo, ari na nia njema hiyohiyo. Mungu Ibariki nchi yetu na watu wake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...