Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Mhandisi Stella Manyanya (wa tatu kutoka kushoto) akikata keki maalum kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Kuongeza Sifa za Kuajirika Kupitia Mafunzo ya Ufundi Stadi (EEVT)kwa mikoa ya Mtwara na Lindi. Uzinduzi huo ulifanywa na Mheshimiwa Naibu Waziri Mhandisi Manyanya, Jumanne, 27 Septemba, 2016 katika chuo cha VETA Mtwara.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Mhandisi Stella Manyanya (wa tatu kutoka kushoto) akikata keki maalum kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Kuongeza Sifa za Kuajirika Kupitia Mafunzo ya Ufundi Stadi (EEVT) kwa mikoa ya Mtwara na Lindi. Uzinduzi huo ulifanywa na Mheshimiwa Naibu Waziri Mhandisi Manyanya, Jumanne, 27 Septemba, 2016 katika chuo cha VETA Mtwara.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Mhandisi Stella Manyanya (wa tatu kutoka kushoto) akila keki na viongozi na watendaji mbalimbali wa taasisi za kiserikali na wadau wa maendeleo kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Kuongeza Sifa za Kuajirika Kupitia Mafunzo ya Ufundi Stadi (EEVT)kwa mikoa ya Mtwara na Lindi. Uzinduzi huo ulifanywa na Mheshimiwa Naibu Waziri Mhandisi Manyanya, Jumanne, 27 Septemba, 2016 katika chuo cha VETA Mtwara.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya, leo Jumanne, 27 Septemba, 2017 amezindua Awamu ya pili ya Mradi wa Kuongeza Sifa za Kuajirika Kupitia Mafunzo ya Ufundi Stadi (EEVT) katika Mikoa ya Mtwara na Lindi. 

Uzinduzi huo umefanyika katika Chuo cha VETA Mtwara.
Katika Mradi huo makampuni ya Mafuta na Gesi chini ya mwamvuli wa mradi wa Kuchakata Gesi Asilia (TLNG) unaojumuisha BG/Shell, ExonMobil, Ophir Energy, Pavilion Energy, na Statoil, yametoa kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 1.9, karibu sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 4, ili kuendeleza mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuajirika, hususani kwa vijana wa mikoa ya Lindi na Mtwara.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Fursa nzuri za utaalam kwenye nchi yetu. Sasa vijana inabidi wahamasishwe kujiunga na shule hizi ili waweze kuwa wataalam wa sekta hii ya mafuta na gesi.
    Pesa iliyochangiwa ni kubwa, serikali inabidi iwe makini kupata walengwa ili hii miraji iwe na tija kwa Taifa.
    Nadhani wanafunzi wachaguliwe kutoka mikoa mbalimbali ili kuweka ushindani wa masomo ili kupata wataalam bora bila kutegema wanafunzi wa Mtwara tu ambao sidhani kama watafikia idadi inayotakiwa.
    Hii sekta ni ngeni hivyo iwe changamoto kwa wanafunzi kuweza kuwa wabunifu na kuelewa masomo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...