WAKAZI wa jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba, 8 hadi 15 wanataraji kuwa katika Dar Restaurant Week ambayo itawawezesha wateja wa migahawa 10 ambayo inashiriki maadhimisho hayo kupata chakula kwa bei pungufu tofauti na ilivyozoeleka.

Akizungumza Mwanzilishi wa Dar Restaurant Week, Adam Senkoro alisema lengo ya kuanzisha maadhimisho hayo ni kupata pesa kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kike ambao familia zao hazina uwezo wa kuwalipia fedha za masomo, na wao watatumia fedha ambazo zimepatikana kwa siku ya ufunguzi kwa ajili ya kuwalipa masomo.
Mwanzilishi wa Dar Restaurant Week, Adam Senkoro akizungumza kuhusu Dar Restaurant Week na jinsi ilivyo na faida kwa wakazi wa Dar.

Alisema ni fursa kwa wakazi wa Dar kutembelea katika migahawa ambayo inashiriki ili kupata chakula wanachokipenda kwa bei nafuu kwa siku zote ambazo zimepangwa mpaka maadhamisho hayo yatakapomalizika.

“Tumeandaa Dar Restaurant Week na mapato ambayo yatapatikana yatakwenda kusaidia kulipa ada kwa watoto wa kike, ninachotaka kuwaambia wakazi wa Dar ni kutembelea migahawa ambayo inashiriki ili kupata chakula kwa bei ndogo,” alisema Senkoro.
Wahudhuriaji wa uzinduzi Dar Restaurant Week wakilipa pesa kabla ya kuingia ndani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kutokana na maadhimisho hayo, Pia vijana wengine wajasiriamali, waliamua kuanzisha mtandao unaoitwa www.mgahawa.co.tz , huu mtandao ni hususan kwa wote wanaotafuta sehem za kula, Kwan migahawa yote ya Tanzania imewekwa kwenye website moja nayo ni http://mgahawa.co.tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...