Katika kukabiliana na upungufu wa ajira hapa nchini Vijana wameshauriwa  kujiajiri  kupitia Sanaa na vipaji walivonavyo katika kupata kipato.

Ushauri huo umetolewa Wilayani  Bagamoyo na Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi alipokuwa anawahutubia wahitimu wa Astashahada na Stashahada  ya Sanaa na Ufundi katika Chuo cha Sanaa na Ufundi  Bagamoyo  kilichopo  chini ya Taasisi ya Sanaa  na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

“Tumieni elimu mliyopata   kujiajiri wenyewe ili kuepuka changamoto ya ajira iliyopo hapa  nchini, ujuzi mliopata  ni njia pekee ya kujiletea kipato na Taifa kwa ujumla”.Alisema  Bibi Leah.

Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa  wasanii wote wanaofanya kazi za Sanaa ni vyema wakasajili  kazi zao katika Mamlaka husika  ili iwe rahisi kwa Serikali  kutoa msaada kwa urahisi kwaWasanii hao.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu waTaasisi ya Sanaa na Utmaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt.Herbet  Makoye aliwasihi  wahitimu hao kuwa mabalozi  wazuri wa sanaa  watakapokuwa wanafanya shughuli zao za Sanaa.

“Nendeni mkawe mabalozi  wazuri wa Chuo  chetu kwa kuwa Wasanii  bora na kutengeneza  kazi nzuri ili muweze kushindana  na soko la ajira”. Alisisitiza Dkt.Makoye.
Naye mhitimu wa ngazi ya  Stashahada ya Sanaa na  Ufundi  Bi Imelda John amesema  kuwa elimu aliyoipata itamsaidia  kufanya kazi ya Sanaa kwa weledi zaidi hasa katika  fani ya kutengeneza Filamu na Picha Jongefu.

Mahafali hayo ni ya 27 katika chuo hicho ambapo kwa mwaka huu jumla ya wanafunzi 85 wametimu Astashahada na Stashahada ya Sanaa na Ufundi. imeandikwa na Shamimu Nyaki- WHUSM.
aimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi akizungumza na wahitimu pamoja na wageni mbalimbali (hawapo pichani) katika sherehe za mahafali ya 27 ya Chuo cha Ufundi na Sanaa Bagamoyo kilichopo chini ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Oktoba mosi Wilayani Bagamoyo. 
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Dkt.Herbet Makoye akisoma hotuba kwa Mgeni Rasmi pamoja na wageni mbalimbali (hawapo pichani) katika sherehe za mahafali ya 27 ya Chuo cha Ufundi na Sanaa Bagamoyo kilichopo chini ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Oktoba mosi Wilayani Bagamoyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...