THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VIJANA WAHIMIZWA KUJISHUGHULISHA KULETA TIJA

TABIA ya vijana kutojishughulisha katika miradi mbalimbali yenye tija kumeeelezwa kuwa moja ya vyanzo vya kudorora kwa uchumi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Allience Mjini Bariadi.

Alisema kumeanza kujitokeza hali ambapo vijana nchini kutokupenda kujishughulisha katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na hivyo kushindwa kuondokana na umaskini na pia kuchangia katika pato la taifa.
Alisema kuwa vijana wanaongoza kwa idadi kubwa lakini wanashindwa kujishughulisha kuhakikisha wanapata maendeleo ambayo yanaweza kulisaidia taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida (kushoto) akisalimiana na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama (kulia) alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi kufungua kongamano la vijana.

Mhagama alisema katika Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Mkoa wa Simiyu, kuratibiwa na Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwamba kuna fursa nyingi lakini vijana wanakuwa wagumu kuzichangamkia na matokeo yake kubaki wakiilalamika serikali kuwa haiwajali.
Alibainisha kuwa serikali itaendelea kusaidia makundi ya vijana yanaoonesha nia ya kujiendeleza

Aidha alifafanua kuwa itawaongezea mtaji wa shilingi milioni 30 kwa kikundi cha vijana cwalioanzisha kiwanda Maziwa cha Meatu pamoja na kile cha Chaki kutokana na jitihada zao walizofanya na matunda kuonekana.
Awali kabla ya kumkaribisha mgeni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema lengo la serikali mkoani hapa ni kuhakikisha linainua pato la mkoa na kuchangia katika pato la taifa kwa kuwawezesha vijana wake kutengeneza bidhaa zinazotokana na malighafi zinazozalishwa mkoani hapa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Naibu wake Mh. Anthony Mavunde wakisalimiana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na ESRF mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Alisema zaidi kwamba wanalengo la kuhakikisha mkoa unaingia katika tano bora ya uchangiaji wa pato la taifa.Amehimiza viongozi kuwasaidia vijana kuwaongoza, kuwaelekeza na amewataka vijana kuwa na uthubutu na kuungana kwa pamoja.Pamoja na harakati za kiuchumi vijana wametakiwa kuwa na mwendo wenye maadili mema ili kuendelea kuwa na afya bora na kukwepa magonjwa yanatokanayo na ukosefu wa maadili.Amesistiza kuwa kauli mbiu waliyoanzisha ya “Bidhaa moja,wilaya moja” itumike ipasavyo ili  kufanikisha maendeleo yao na ya wilaya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.