THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Vijana wasomi 53 wafyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni na nyumba za walimu Shule ya SeKondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani

 Vijana wasomi 53  wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani, umbali wa kilomita 151 kutoka Dar es salaam, na kilomita 53 kutoka makao makuu ya Wilaya. 
Vijana hao ni wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali nchini  na nje ya nchi ambao wamejitolea kufnya kazi hiyo nzito bila malipo.
Vijana hao, ambao wameungana katika  grupu la Whatsapp la WAZALENDO,  leo wamekutwa wakifanya kazi hiyo nzito huku wakihamasika kwa nyimbo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga (wa pili kulia). 
Vijana hao, 14 wakiwa wanawake na 39 wanaume, walikubaliana kupiga kambi shuleni hapo toka Septemba 27, 2016  na kufanya kazi hiyo ya kujitolea na bila malipo kwa moyo mmoja na kufanikiwa kufyatua matofali hayo. Kambi hiyo inatarajiwa kufungwa kesho Jumamosi Oktoba 29, 2016 na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako.
 Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
 Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akipungia pamoja  na vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.

Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    I'm proud of you all, ninyi ni wazalendo wa kweli.
    Badala ya kukaa na kusubiria pres. Magufuli ataifanyia nini Tanzania, nyie mlijiuliza mtaifanyia nini nchi yetu. Magroup mengine ya whatsapp igeni mfano huu na kuwa productive badala kupiga siasa maandazi na kulaumu serikali kwa kila kitu. Bravoo

  2. Anonymous Anasema:

    Safi sana bwana michuzi. Hiyo shule niliitembelea mara 2 kati ya 2004 na 2006 kwaajili ya utafiti wa ELIMU NA MAZINGIRA kwa mtoto wa kike. Hali ya shule hiyo ilikuwa mbaya sana na walimu hawakuwa na nyumba. Wazalendo hawa ni Nyerere type. I big up them.