THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VIJANA WATAKIWA KUACHA KILA MARA KUIHOJI SERIKALI NA BADALA YAKE WAJIKITE ZAIDI KUFANYA KAZI

Kufuatia changamoto ya uhaba wa ajira hususani kwa vijana nchini, wametakiwa kuwa wabunifu na watafutaji wa fursa za kujiajiri badala ya kuilalamikia serikali kuwa haitatui changamoto hiyo kwa muda mrefu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza katika Kongamano la Vijana lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam kuelekea sherehe za maadhimisho ya wiki ya Umoja Mataifa, amesema vijana inabidi wawajibike katika kuleta maendeleo ya uchumi kwenye jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumla.

Pia amesema vijana waache kuhoji serikali kuwa inawafanyia nini badala yake wawe wazalendo kwa kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya Taifa lao.
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC). (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

"Tuna kazi kubwa ya kujenga fikra za vijana kwamba ili kufanikiwa katika maisha siyo lazima kuajiriwa, vijana wengi ukiwahoji wanakwambia changamoto kubwa wanayoikabili ni ukosefu wa ajira. Lakini wanasahau kuwa changamoto zipo nyingi zinazowakabili," amesema.

Prof. Ole Gabriel amezitaja changamoto nne zinazokabili vijana ambazo zinasababisha washindwe kujiajiri au kushindwa kujiendeleza pindi wanapojiajiri kuwa ni, ukosefu wa fikra kutokana kwamba wengi hawaziruhusu fikra zao kubuni mbinu za kujiajiri. Changamoto nyingine aliyoitaja ni vijana kukosa uelewa, mbinu na ubunifu wa kuongeza thamani ya shughuli wanazofanya.

Changamoto nyingine aliyoitaja ni mfumo mbovu na usio rafiki kwa vijana hasa mifumo duni ya upatikanaji mitaji na masoko, hususani katika kipindi hiki ambacho kuna wimbi kubwa la vijana wasio na ajira.
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo kwa vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo.

Ameshauri kuwa "Hivi sasa kuna elimu ya ujasiriamali lakini niseme tu haitomsaidia kijana kujikwamua sababu hutoa elimu ya uzalishaji pekee. Ili kijana afanikiwe na ujasiriamali, kwanza inabidi apewe elimu ya kufanya utafiti wa bidhaa inayohitajika kwa kipindi husika, akishajua bidhaa hitajika ndipo afanye uzalishaji kisha hatua ya mwisho kutafuta masoko ambayo tayari ameshayafanyia uchunguzi."

Pia ameshauri vijana kuwekeza katika biashara kilimo kwa kuwa ndiyo sekta pekee yenye fursa ya kutoa ajira kwa wingi kwa kuwa imeajiri asilimia 84 ya vijana.

"Tanzania ina vijana zaidi ya milioni 16.2 ni sawa na asilimia 70 ya watanzania, waliofanikiwa kuajiriwa katika sekta binafsi ni milioni 1, waliojiajiri milioni 1.1 waliopo katika sekta ya umma ni 18,8000 na katika sekta ya kilimo wapo vijana milioni 13.2 na bado nafasi zipo katika sekta hiyo," amesema.
Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza machache kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
MC maarufu nchini ambaye pia ni Mhamasishaji Ujasiriamali, Anthony Luvanda akizungumzia ajira yake binafsi na mafanikio aliyonayo kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA