VIJANA Wawili ambao majina yao hayakutambulika mara moja, wamejikuta katika mikono ya wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kupora kupora mali katika eneo la Barabara ya Mawaziri karibu na Nyumba za TPDC, Mikocheni Jijini Dar e salaam.

Kwa mujibu mashuhuda wa tukio hilo, inaelezwa kuwa Vijana hao ambao walikiwa na usafiri wa Bajaj, baada ya kufanya tuiko hilo la uporaji wakawa wanakimbia kuelekea upande wa kwa Warioba ila kwa bahati nzuri kuna kijana mkata majani aliwaona na kuamua kuwakimbiza kwa Baiskeli huku akipiga yowe la "Wezi Wezi" na ndipo watu wakatoka na kuizuia Bajaj hiyo na kuanza kuwatembezea mkong'oto mpaka pale Askari wa Jeshi la Polisi walipofika na kuwachukua.

Inaelezwa kuwa eneo hilo lina vijana wengi sana wanaofanya matukio ya uporaji huku wahanga wakubwa wakiwa ni wanafunzi wa chuo cha Kodi cha TRA.
 Mmoja wa vijana hao akipandishwa kwenye gari ya Polisi baada ya kupokea kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.
 Usafiri waliokuwa nao vijana hao.
 Inadaiwa kuwa hii silaha alikuwa nayo mmoja wa vijana hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...