Makamu Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Bara, Mhe. Phillip Mangula akiwasilisha mada kuhusu
Maadili ya Viongozi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za
Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam katika
ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo
yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl.
Nyerere afariki dunia.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akimpongeza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mhe. Phillip Mangula mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu Maadili ya Viongozi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA).Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila, Mwenyekiti wa Kongamano hilo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri msaafu Mhe. Anne Makinda.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano
la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere wakifuatilia mada
kutoka kwa wawasilishaji ambao ni Mhe. Phillip Mangula, Joseph Butiku,
Ibrahim Kaduma na Dkt. Harun Kondo, mada zilizowasilisha ni pamoja na
Miiko ya Uongozi, Azimio la Arusha na Maadili ya Viongozi.
Mchumi Mwandamizi Profesa Ibrahim
Lipumba akichangia mada wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi
za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam katika
ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho
hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa
Mwl. Nyerere afariki dunia.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kongamano la
Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere(MNMA) akiagana na washiriki.Picha na. Frank Shija, MAELEZO.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...