Wabunifu mitindo waonesha mavazi uzinduzi duka la maharusi Na Mwandishi Wetu WABUNIFU wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi wamejitokeza kufanya maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi katika uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaa. Uzinduzi huo uliofanyika jana eneo la Sinza Madukani ulipambwa na mbunifu wa mitindo kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kwa jina la Femi, mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa ambao ni waandaaji wa onesho alisema waliamua kufanya onesho hilo ili kutoa fursa kwa wananchi hasa wanaoelekea kufanya harusi kujua mitindo mbalimbali ya mavazi ambayo wanaweza wakaitumia katika shughuli zao za harusi na kuonekana tofauti kimuonekano.

Alisema wabunifu walifanya maonesho ya mavazi katika mitindo mbalimbali kutumia mavazi ya hali zote ikiwa ni kuonesha jamii harusi si lazima muhusika au maharusi kutumia gharama kubwa bali wanaweza kutumia gharama za chini na kuonekana wenye mvuto kama watapata ushauri kutoka kwa wabunifu na wanamitindo. 

Alisema duka lao pamoja na kuuza nguo za maharusi watakuwa wakitoa ushauri bure kwa maharusi endapo watafika katika duka hilo ambalo limekuja kuleta mabadiliko katika mitindo ya maharusi. Alisema duka hilo litahudumia watu wenye kipato cha chini, cha kati na hata cha juu kulingana na mahitaji ya wahusika huku wakinufaika kwa ushauri bure kila atakaetembelea na kuomba ushauri kwa wataalamu wa mitindo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mmiliki wa duka hilo, Mary Monyo pamoja na Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa (kulia). Uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani ulikwenda sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi toka Tanzania.
Mmiliki wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana, Mary Monyo (kulia) akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria.
Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kushoto) akimlisha keki Mwendeshaji wa duka hilo, Victoria Chuwa (kulia) mara baada ya uzinduzi wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam.
Mbunifu maarufu wa mitindo kutoka nchini Nigeria, Femi (wa pili kushoto), pamoja na mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano (wa kwanza kulia) wakiwa katika pozi pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania, kwenye maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanyika katika duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...