Kaimu Kamishna Generali wa Idara ya Uhamiaji ya Uhamiaji, Victoria Lembeli, akipokea Kombe  la ushindi wa klabu Bingwa Taifa kutoka kwa Nahodha wa timu ya Uhamiaji , Neema Massawe wakati wa hafla ya kuwapokea wachezaji wa timu hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa timu ya Idara ya Uhamiaji wakiingia katika Ofisi za makao makuu ya Idara hiyoKurasini jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wa Ngazi ya juu wa Idara ya Uhamiaji wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishiwahabari.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Na  Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
WITO umetolewa kwa timu ya mchezo wa mpira wa pete ya Idara ya Uhamiaji nchini kuongeza juhudi katika michezo mbalimbali hili kuimarisha umoja na mshikamano uliopo nchini.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini , Victoria Lembeli, alipokuwa akipokea kikombe cha ushindi wa Klabu bingwa Taifa kwa timu ya mpira wa pete

“Hakika niwapongeze kwa ushindi mliopata kwani mmeweza kushindana katika ,mazingira magumu hivyo nilivyopata kusikia kuwa mmekuwa mabingwa sikuamini masikio yangu hivyo naomba muendelee na moyo huo huo kwa kuwa michezo ndio inadumisha umoja na mshikamano” anasema
Kamishna Lembeli aliongeza kuwa mshikamano na juhudi katika michezo viatachangia kuongeza utashi wa kazi .

Kwa uapande wake Nahodha wa timu hiyo ,Neema Massawe alisema kuwa wao kamatimu wamejipanga kushinda mishandano yote yaliyo mbele yao hili kuendelea kutetea nafasi walizonazo.

Alitamba kuwa Uhamiaji ndio timu pekee inayofanya vizuri katika mchezo wa mpira wa pete hapa nchini hivyo tasisi nyingine za serikali na majeshi zinapaswa kujipanga na kujifua sana hili kufikia wao walipo.

Aliongeza kuwa wameweza kucheza mashindano ya Klabu bingwa Taifa bila ya kufungwa hata mchezo mmoja na timu zote 12 jambo ambalo linathibitisha ubora wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...