NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID

WADAU kutoka kada mbalimbali wamekutana kujadiliana jinsi sekta binafsi itakavyoshiriki katika utekelezaji thabiti wa mpango wa pili wa miaka mitano wa maendeleo ya Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, amesema sekta binafsi inao umuhimu mkubwa katika kushiriki kuandaaa na kujadili mipango mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Kida aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Warsha ya majadiliano kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika kutekeleza mpango wa pili wa miaka mitano wa maendeleo ya Tanzania, (FYDP II) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na ESRF, Serikali kupitia Tume ya Mipango na Mpango wa Kusaidia Mabadiliko ya Kiuchumi, (SET), iliwakutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, (TPSF), CEO roundtable, Suma JKT, Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) , wadau wa maendeleo kutoka Jumuiya ya Ulaya, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na wasomi.

Dkt. Kida alisema, Majadiliano hayo nimatokeo ya juhudi zilizoanza tangu 1998-200, ambapo ESRF ilishiriki katika uanzishwaji wa mpango wa Taifa wa Vision 2025 uliolenga kuitoa Tanzania kwenye kundi la nchi masikini hadi zile zenye uchumi wa Kati, (Middle income coutry.

“Mwaka 2011 ESRF ilifanya mkakati wa kupitia mpango huo wa vision 2015 na kubaini masuala kadhaa ambayo yalihitaji kuelezewa kama kweli taifa linaelewa mpango huo wa kipindi kirefu.” Alisema na kuongeza ni hivi karibuni sisi katika ESRF tulifanya mapitio ya mkakatiwa kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDPI), na MKUKUTA II, mapitio ambayo yamechangia kuingia katika Mpango huu wa pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, (FYDP II), Alisema Mkurugenzi huyo Mtendaji wa ESRF.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, (kulia), akizungumza kwenye Warsha ya majadiliano ya wadau kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika kutekeleza mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano (FYDPII), kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoawa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka
Naibu Katibu Mkuu Tume ya Mipango, kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango, Dkt. Maduka Paul Kessy(kushoto0, akizungumza kwenye warsha hiyo. 
Mkurugenzi wa Huaduma kwa Wanachama, Taasisi ya Sekta Binafsi, (TPSF), Bw. Louis Accaro, akitoa mada yake juu ya sekta za kipaumbele ambazo zinapaswa kujadiliwa ili kufanyiwa kazi, sekta hizo ni kutoka zao la Pamba na kuwa nguo, kutoka ngozi na kuwa mazao yatokanayo na ngozi, na pia viwanda vya madawa
Baadhi yawashiriki wa warsha wakifuatilia mjadala

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka, akizungumza wakati wa warsha hiyo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...