THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAFADHILI WAFURAHISHWA NA UKAUSHAJI WA MBOGA MBOGA MKOANI MOROGORO

Mkurugenzi wa mawasiliano wa taasisi ya Mfuko wa Wanawake Afrika, Anna Salado (kulia), akipakua mboga zilizopikwa kiasili na kuungwa kwa nazi wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea mradi wa ukaushaji wa mboga na matunda wa wanawake wa Kata ya Mzinga mkoani Morogoro hivi karibuni. Kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Milikieli Mansweat Mahiku.
Mratibu wa mradi wa Green Voices kutoka taasisi ya Mfuko wa Wanawake Afrika ya Hispania, Alicia Cebada, akiwa ameshikilia pakiti ya kisamvu kilichokaushwa na kufungashwa huku akiwapongeza wanawake wa kikundi cha Mzinga katika Kata ya Mzinga, Manispaa ya Morogoro kwamba wamefanya kazi nzuri sana. Mwenye fulana nyeupe ni Bi. Esther Muffui, mshiriki kiongozi wa mradi huo.

SIYO tu mapishi ya asili ya kisamvu kikavu kilichoungwa kwa nazi, lakini mafanikio makubwa katika ukaushaji na usindikaji wa mboga na matunda katika mradi wa wanawake wa Kata ya Mzinga, Manispaa ya Morogoro yamewavutia wahisani wa taasisi ya Women for Africa Foundation kutoka Hispania.

Hali hiyo imewafanya wanawake hao wawe katika nafasi kubwa zaidi ya kusonga mbele ikiwa wafadhili hao watatoa tena fedha katika awamu ya pili ya mradi wa Green Voices unaotekelezwa nchini Tanzania.

Akizungumza katika Kijiji cha Konga kwenye Kata hiyo, mratibu wa mradi huo kutoka Hispania, Bi. Alicia Cebada, alisema kwamba licha ya kuwa na muda mfupi tangu kuanza kwa mradi huo, lakini wanawake hao wamefanya mambo makubwa ambayo yanastahili kuungwa mkono.