WAFANYABISHARA Mkoani Shinyanga, wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kusajili majina ya biashara zao katika zoezi linaloratibiwa na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) ili waweze kutambulika kisheria na kuchangia mapato ya Serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Bi. Zainabu Telack, amewahamasisha wafanyabiashara mkoani humo kutumia fursa ya kuwepo maofisa wa BRELA kutoka makao makuu ya BRELA kurasimisha biashara zao na kujifunza umuhimu wa kusajili majina ya biashara.

“Tumepata bahati kubwa kutembelewa na maofisa wa BRELA ambao wanaendesha semina kwa wafanyabiashara na wakati huo huo kusajili majina ya biashara,” Bi.Telack alisema hayo mkoani hapa jana wakati wa semina ya wiki moja ya uhamasishaji wa usajili majina ya biashara inayoratibiwa na BRELA.

Alisema azima ya serikali ya Awamu ya Tano ni kuwekeza katika biashara na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa lengo kubwa kukuza uchumi wa taifa, kuongeza ajira na kukuza kipato cha watanzania.

“Napenda kuchukua nafasi hii pia kuwashukuru na kuwapongeza BRELA kwa zoezi ili la uhamasishaji kwani ni matumaini yangu mwitikio utakuwa mkubwa sana,” alisema na kuongeza kuwa Shinyanga itakuwa mfano wa kuigwa katika urasimishaji biashara.

Afisa mtendaji mkuu wa BRELA, Frank Kanyus, akiainisha faida za usajili wa biashara, amesema pamoja na mambo mengine kutasaidia serikali kupata mapato ili iweze kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi, alisema Wakala umejipanga na zoezi la kuzunguka nchi nzima kutoa elimu na faida za kusajili majina ya biashara nchi nzima.

“Mikoa ambayo tumeshafanya semina tulipata mwitikio mkubwa na pia watu wengi walijitokeza kusajili majina ya biashara zao,” alisema na kuongeza kuwa wakala ataendelea kuwahamasisha wafanyabiashara kurasimisha shughuli zao.Alisema tayari BRELA imeshatoa semina katika mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu na Geita ambapo wiki ijayo semina za uhamasishaji zitafanyika mkoani Tabora.

Naye, Afisa Mtendaji wa Chama cha wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Mkoani Shinyanga, Bi.Malicelina Saulo,alisema jumuiya ya wafanyabiashara imefuruhishwa na semina yenye lengo la kuwajengea uelewa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kusajili majina ya biashara zao.

“Hii ni fursa pekee kwa wafanyabishara mkoani Shinyanga kujisajili majina ya biashara zao na kuwaondolea usumbufu wa kusafiri umbali mrefu hadi Dar es salaam,” alisisitiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...