Afisa Mipango wa Bodi ya Filamu Tanzania Mfaume Said akiwasilisha mada inayohusu historia, majukumu na mipango ya baadae ya bodi hiyo mbele ya wasanii wa kike waliohudhuria mafunzo ya kuongeza ushiriki wao kwenye tasnia ya filamu. Mafunzo hayo ya siku mbili ni mwendelezo wa juhudi za Bodi ya Filamu kuongeza ubora wa filamu za Kitanzania.
Mkufunzi Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam Dkt. Mona Mwakalinga akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada inayohusu njia mbalimbali zinazotumika kuongeza uwezo wa mwigizaji kuuvaa uhusika kwenye michezo ya kuigiza na filamu.
Baadhi ya waigizaji wanaoshiriki mafunzo ya siku mbili ya kuwaongezea ushiriki waigizaji wa kike wakifuatilia mada inayowasilishwa na Mkufunzi Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam Dkt. Mona Mwakalinga. Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika ukumbi wa Habari Maelezo, jijini Dar-es-salaam
Mwigizaji wa michezo ya kuigiza na filamu Bi. Madina Mjatta (Zawadi) akichangia mada wakati wa mafunzo ya siku mbili yanayolenga kuongeza ushiriki wa waigizaji wa kike kwenye tasnia ya filamu nchin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...