jioni maeneo ya Salasala Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Polisi wakishirikiana na Kikosi kazi cha kuzuia uharibifu wa miondo mbinu ya Shirika la umeme Tanzania Tanesco lilipata taarifa toka kwa raia mwema kuwa kuna watu wanaohujumu miundo mbinu ya Shirika hilo.

Kikosi hicho kilifika eneo hilo katika nyumba ya Willfred Barutti (45) mkazi wa Makumbusho na kufanya upekuzi kwenye nyumba hiyo ambapo walivipata vifaa mbalimbali Line Meterial ambavyo hutumika kwa ajili ya kuunganisha umeme vya Kampuni ya Tanesco.Polisi walikwenda katika nyumba nyingine mali ya Betrice Emmanuel (42) mkazi wa Salasala Mabanda wakafanya upekuzi na kufanikiwa kukamata vifaa vifuatavyo;

Nyaya aina ya Drums'02,roller ya waya aina ya AICC ya umeme wa 50 mm ambazo hutumiwa na tanesco kituo cha Kilimahewa huko Kawe Wilaya ya Kinondoni.

Thamani ya vifaa hivyo vinakadiliwa kuwa Tsh.61,000,000,Watuhumiwa wawili wanashikiliwa kwa mahojiano na Upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani 
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Leila Muhaji akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wizi huo wa vifaa vya umeme vyenye thamani ya milioni 61 na kukamatwa,Kulia ni Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.
Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.(wa pili kushoto) akiwa na waandishi. 
Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.(wa pili kushoto) akiwa na waandishi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...