THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Wakazi wa Dar washauriwa kushiriki zoezi la unywaji dawa za magonjwa yasiyopewa kipaumbele

WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam washauriwa kuchangamkia fursa ya zoezi la Unywaji dawa za magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele kwa jamii ili waweze kujikinga na magonjwa hayo.  

Magonjwa hayo ni pamoja Mabusha, matende, usubi, Minyoo zitakazo kuwa zinatolewa katika vituo vya afya vyote vya mkoa pamoja na kwenye mikusanyiko ya watu.

Akizungumza leo katika uzinduzi wa zoezi hilo la unywaji wa dawa hizo litakalochukua siku tano kwa mganga mkuu wa mkoa Grace Magembe amesema wagonjwa watakaopatikana na tatizo hilo la watafanyiwa upasuaji.

“Tumeandaa vituo vya afya pugu, na Mbweni mission ambako upasuaji utakuwa unaendelea huku tukishirikiana na madaktari kutoka hospitali ya Muhimbili.”

Ameongeza kuwa mpaka sasa zoezi la upasuaji litaendelea hadi mwezi wa 12 mwaka huu, ambapo mpaka hivi sasa zaidi ya wagonjwa 104 wameshafanyiwa upasuaji.

“Zoezi hili tumelipa sana kipaumbele ili kuokoa nguvu kazi ya taifa, tumeandaa vituo zaidi ya 281 kwa ajili ya zoezi  hili wanaume kwa wanawake wajitokeze kumeza dawa hizi”.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wananchi kuepuka maneno yayozungumzwa mitaani kuwa dawa zinamadhara hivo kujitokeza kumeza dawa ili waepukanae na magonjwa hayo.

“Zoezi linaendelea vyema watanzania wajitokeze, pia na zoezi la usafi liendelee ili kuepuka mazalia ya mbu ambao ni vigumu kuwatambua wanaeneza ugonjwa huu’’.

Wizara ya afya na ustawi wa jamii inaendesha zoezi hili kuanzia mwaka 2009, huku kwa mkoa wa Dar es saam wakitarajiwa kuwafikiwa wananchi zaidi ya milioni 4 , ili kuwakinga na magonjwa hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiongea na wananchi kujitokeza katika zoezi la unywaji wa dawa leo jijini Dar es salaam.
Mganga mkuu wa Mkoa Grace Magembe akihimiza wananchi kuhusu kujitokeza kupata chanjo ya Mabusha na Matende jijini Leo.