Katibu tawala wilaya ya Chemba,Ndugu Nyakia Ally
Katika kuadhimisha kumbukizi ya miaka 17 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere, Maadhimisho ya kilele cha wiki ya Vijana pamoja na Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru hapo kesho tarehe 14/10/2016. 

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Ndugu Nyakia Ally,alipokuwa akizungumza na Globu ya Jamii kwa njia ya Simu,leo.

Nyakia amesema kuwa Wilaya ya Chemba imepanga kufanya yafuatayo katika kuenzi harakati na juhudi za Muasisi huyu wa Taifa letu.

Ikumbukwe Mwl Nyerere katika maisha yake alipigania ukombozi wa Tanzania katika 1.  Kupambana na adui ujinga. 2. Adui Maradhi. 3. Adui Umasikini na 4. Adui njaa.

"Hivyo Wilaya yetu itaadhimisha siku hii kwa kushiriki kwa kusafisha eneo itakapojengwa Zahanati ya Wilaya ya Chemba na wananchi watachangia matofali ya ujenzi wa Zahanati hiyo. Vile vile zoezi hilo litaendana na uchangiaji wa damu katika benki ya damu hapa Wilayani Chemba",alisema Nyakia

Amesema kuwa baada ya kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kijamii,baadae Kutakuwepo na Michezo mbalimbali ya kuvuta kamba  baina ya Watumishi wa Serikali na Wananchi wa Kijiji cha Chemba,Kukimbiza kuku na mwisho kutakuwa na mchezo wa bao kati ya Wazee wa hapa Chemba katika kumuenzi Mwl Nyerere ambaye alikuwa mpenzi mkubwa wa mchezo huu.

Amesema kuwa Washindi katika mchezo wa kuvuta kamba na nao watajinyakulia zawadi ya Mbuzi na ule wa kukimbiza kuku kwa upande wa wanawake na wanaume watajinyakulia kuku watakaye mkamata.

Katibu Tawala wamewaomba wananchi wa Chemba na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi bila kukosa katika tukio hili la kipekee la kuenzi juhudi za Baba wa Taifa katika kuwaletea wananchi maendeleo majira ya saa 2:00 asubuhi ya kesho katika viwanja vya michezo shule ya Msingi Chemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...