Na John Gagarini, Mkuranga

WANANCHI wametakiwa kuwa na utamaduni wa kulipa kodi mbalimbali za serikali ili ziweze kutumika kwa ajili ya maendeleo kama wanavyofanya wananchi wa Libya.

Hayo yalisemwa wilayani Mkuranga na mkurugenzi wa Taasisi ya World Islamic Call Society iliyopo chini ya ubalozi wa Libya hapa nchini Ammara Zaiyani wakati akikabidhi mradi wa kisima cha maji kwenye Kijiji cha Binga–Kisiju.Zaiyani alisema kuwa fedha ambazo zimesaidia ujenzi wa kisima hicho cha maji ya kunywa chenye thamani ya shilingi milioni 18 zimetokana na kodi za wananchi wa Libya kwa ajili ya kusaidia watu wenye changamoto mbalimbali za kimaendeleo.

“Wananchi wa Libya wanajitolea kuwasaidia wenzao hivyo na nyie mnapaswa kuwa na utamaduni wa kuwasaidia wengine kupitia kwenye malipo mbalimbali ya serikali yenu ambayo ina sema hapa Kazi Tu,” alisema Zaiyani.Naye mwakilishi wa Ubalozi wa Libya hapa nchini Mohamed Atoumi alisema kuwa serikali ya Libya kupitia taasisi hiyo imekuwa ikipokea maombi mbalimbali na imekuwa ikisaidia kadiri ya uwezo unapokuwepo.

Atoumi alisema kuwa wamekuwa wakisaidia kwenye sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja kwenye huduma za afya, maji na shughuli nyingine za maendeleo lengo likiwa ni kudumisha ushirikiano uliopo na Tanzania.

Kwa upande wake kadhi mkuu wa mkoa wa Pwani Sheikh Hamis Mtupa alisema kuwa wanashukuru kwa msaada huo kwani umesaidia kuwaondolea adha wananchi wa Kijiji hicho ambao walikuwa wakishinda wakitafuta maji ambayo siyo safi wala salama.

Mtupa alisema kuwa wananchi wanapaswa kulinda miundombinu ya kisima hicho ili isiharibike kwani maji hayo ni kwa wananchi wote bila ya kujali dini ya mtu na ni huduma muhimu kwa binadamu.Naye mkazi wa kijiji hicho Mwanahawa Maulid alisema kuwa wamekuwa wakihangaika kutafuta maji ambayo yanapatikana mbali na wamekuwa wakitumia muda mwingi kusubiria maji.

Maulid alisema kuwa maji waliyokuwa wakiyatumia ni ya kuchimba chini ambayo si salama kiafya na yamekuwa wakiwasababishia magonjwa mbalimbali kama vile kuhara na UTI.
Mkurugenzi wa Taasisi ya World Islamic Call Society ya Libya tawi la Tanzania Ammara Zaiyani kulia aliyeshika ndoo ya maji baada ya kumtwisha ndoo ya maji Saida Ally mkazi wa Kijiji cha Binga-Kisiju kata ya Dondo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, kushoto kadhi mkuu wa mkoa wa Pwani Sheikh Hamis Mtupa (Picha na John Gagarini).
Mkurugenzi wa Taasisi ya World Islamic Call Society ya Libya tawi la Tanzania Ammara Zaiyani akifungua bomba la maji baada ya uzinduzi wa kisima cha maji kwenye Kijiji cha Binga-Kisiju wilayani Mkuranga mkoani Pwani kushoto kwake ni mwakililishi wa balozi wa Libya Mohamed Atoumi
Mkurugenzi wa Taasisi ya World Islamic Call Society ya Libya tawi la Tanzania Ammara Zaiyani katikati akielezea jambo kulia ni kadhi mkuu wa mkoa wa Pwani Sheikh Hamis Mtupa na kushoto ni mwakililishi wa balozi wa Libya Mohamed Atoumi wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji kwenye Kijiji cha Binga Kisiju- kata ya Dondo wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani Picha na (John Gagarini)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...