Na Editha Karlo, wa blog ya jamii,Missenyi
SHULE
ya msingi Byamutemba iliyopo katika kata ya Nsunga Wilayani Misenyi
imefungwa kwa muda wa wiki tatu,kufuatia shule hiyo mapaa yake kuezuliwa na upepo mkali.
Tukio hilo limetokea leo majira ya mchana wakati wanafunzi wakiendelea na
masomo darasani na kusababisha baadhi ya wanafunzi kujeruhiwa.Upepo huo umeezua mapaa ya shule hiyo nyumba moja ya mwalimu pamoja na nyumba tatu za wakazi wa kijiji cha Byamutemba.
Mganga
msaidizi wa Wilaya ya Missenyi Godon amekiri kupokea wanafunzi hao
waliojeruhiwa 14 na wanafunzi 7 wakirudishwa nyumbani baada ya kupatiwa
matibabu kwenye Zahanati ya Igayaza.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Luteni Kanali Denis Mwila alisema kuwa
wameifunga shule hiyo kwa miezi mitatu wakati wanafanya utaratibu wa
kuijenga shule hiyo kwa haraka.
Alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 903.
Shule
ya msingi Byamutemba iliyoko kata Nsunga Wilayani Missenyi imeezuliwa
na upepo mkali na kupelekea Wanafunzi saba kujeruhiwa,kufuatia tukio
hilo, shule hiyo kwa sasa imefungwa kwa muda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...