THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Wanaharakati Wakutana kuiomba serikali kufuta adhabu ya Kifo

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii.

Wanaharakati na wadau wa sheria wamekutana leo jijini Dar, kupinga adhabu ya kifo na kuiomba Serikali kutafuta adhabu mbadala na kubadilisha sheria hiyo kwakuwa ipo kinyume na haki za Binadamu.

Akizungumza wakakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililondaliwa na kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC) katika ukumbi wa British Council Dar es Salaam, Kamishina wa tume ya haki za Binadamu na utawala bora nchini ,Tom bahame Nyanduga amesema kuwa serikali inapaswa kuangalia upya sheria hiyo kwa sababu ni kandamizi na ni ya kikoloni.

"Nchi zaidi ya ishirini Barani Afrika zimeshafuta sheria hii na nchi kama za Umoja wa Ulaya na Canada sheria hii haitumiki ,hivyo serikali inapswa kuangalia upya namna ya kufuta sheria hii kwakuwa haitekelezeki ,kwani licha ya watu kuhukumiwa ni miaka 20 sasa imepita hakuna mtu aliyeweza kunyongwa hapa nchini"amesema Nyanduga.

Aliongeza kuwa adhabu hiyo ipo kinyume na haki za binadamu na inapingana na katiba ya nchi inayosema kila mmoja ana haki ya kuishi na ikitekelezwa aina adhabu mbadala na kuwafanya watu kuishi kwa wasiwasi wakiwa magerezani.

Alitolea mfano nchi kama Afrika Kusini na Rwanda licha ya kukithiri kwa mauji ya watu bado zimekubali kufuta adhabu hii ambayo inatoa utu wa mtu na kumnyima haki ya kuishi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC),Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa kwa pamoja tunapaswa kuungana kupinga adhabu hii ambayo inatekelezwa kwa makosa matatu tu hapa nchini.

Ametaja kuwa adhabu hii inatekelezwa kwa makosa ya Mauaji,Uaini na wanajeshi ambao wameasi nchi na kwenda na kinyume nataratibu na kanuni za majeshi yetu .Ameweka wazi kuwa kwa mujibu ya maoni ya wadau na wananchi ni asilimia 50% tu ndio waliomba kuendelea kuwepo kwa adhabu hii huku wengine wakikataa adhabu ya kifo.

Amesema kuwa kuna uelewa mdogo wa jamii juu ya adhabu ya kifo nchini kutokana na mitazamo tofauti Imani na Mila na desturi za makabila mbalimbali.
Mkurugenzi wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu Hellen Kijo Bisimba ,akizungumza na wadau walioshiriki Kongamano hilo, kulia ni Kamishna wa Tume yanhaki za Binadamu na utawala bora nchini Bahame Nyanduga ,kushoto kwake ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini,Rodvel Vd Ges.
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora,Tom Bahame Nyanduga akizungumza na washiriki katika kongamano hilo.
Washiriki na wadau mbalimbali walioudhuria kongamano hilo katika ukumbiwa Britisha Council Dar es Salaam.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Ibrahim Dahal Anasema:

    Hukumu ya kifo inategemea na kosa, kama mtu ameua kwa kukusudia huyo naye lazima auawe. Kwanza angalieni haki za wanaodhulumiwa kabla ya kuwatetea madhalimu.