Na Grace Michael, Simiyu.

HUDUMA za upimaji afya bure zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayokwenda sambamba na tukio la uzimaji Mwenge zimekuwa kivutio kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu.

Mfuko unatoa huduma za vipimo vya shinikizo la damu, kiwango cha sukari, uzito na urefu lakini pia mwananchi anayepima anapata fursa ya kupata elimu ya namna ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza kwa kuzingatia mtindo bora wa maisha.

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti bandani hapo, wananchi hao wamesema, kitendo kilichofanywa na Mfuko cha kusogeza huduma hiyo mkoani humo ni nzuri kwa kuwa inawapa fursa ya kujua hali ya afya yao.

“Kwa kweli niwapongeze sana kwa huduma hii ambayo mnatupima bila ya kutoa gharama yoyote lakini kitu kizuri Zaidi ni kupata elimu ya namna ya kuishi ili kuepukana na maradhi ambayo yanaweza kuepukika kwa kuzingatia ushauri wa wataalam ambao leo tunaupata bila gharama yoyote,” alisema Bw. Maduhu Sita mkazi wa Bariadi.

Akizungumzia mwitikio wa wananchi bandani hapo ambao wanafika kwa lengo la kupata huduma ya vipimo, Meneja wa NHIF Mkoa wa Shinyanga na Simiyu Bw. Imanuel Amani alisema kuwa mwitikio wa wananchi ni mkubwa sana.

“Mwitikio kwa kweli ni mkubwa sana nah ii inaonesha tu kwamba wananchi wanataka kujua hali ya afya zao na kwa upande wetu NHIF tupo tayari kuwahudumia hawa wananchi kwa kadri itakavyowezekana hivyo hata ambao hawajafika hapa waje ili tuwahudumie,” alisema.

Alieleza kuwa mbali na upimaji wa afya, Mfuko pia unatumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi kujiunga na huduma zake ili wawe na uhakika wa kupata matibabu wakati wowote. 

“Kwa sasa NHIF imepanua wigo wake ambapo makundi mbalimbali yanaruhusiwa kujiunga na huduma zake yakiwemo makundi ya wajasiliamali, watoto, wanafunzi, watu binafsi hivyo nawaomba wananchi wafike bandani kwetu ili tuwahudumie,” alisema Bw. Amani.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka akipima kipimo cha shinikizo la damu wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwenye maonesho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea mkoani humo.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Imanuel Amani akitoa elimu kwa wananchi waliofika bandani hapo kujua huduma zinazotolewa na Mfuko.
Maofisa wa NHIF wakiendelea na kuwahudumia wananchi waliofika bandani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...