Na Ally Daud-MAELEZO

WANANCHI waaswa kutoa taarifa pale wanapohisi wamepata madhara ya dawa wanazozitumia ili kuirahisishia Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuchukua hatua stahiki zidi ya watengenezaji wa dawa hizo ili zisiendelee kuwadhuru wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwenye hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa uliofanyika jijini Dar es salaam.

Waziri Ummy amesema kuwa wananchi wawe mstari wa mbele katika kutoa taarifa pindi wanapohisi kupatwa na madhara ya dawa wanazozitumia ili kuirahishia TFDA kuchukua hatua stahiki kutokana na taratibu na sheria zilizopo za kuondoa madawa feki nchini.

“Napenda kusisitiza kwa wananchi wote kutoa taarifa pale wanapohisi wamepata madhara ya dawa ili kuirahishia TFDA kuchukua hatua stahiki kutokana na utaratibu na sheria zilizowekwa” alisema Waziri Ummy.
Afisa wa Uthibiti wa Majaribio na Usalama wa Dawa (TFDA)Dkt. Alex Nkayamba kushoto akimpa maelekezo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kuhusu mfumo wa wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa unavyopatikana kwenye simu za mkononi wakati wa hafla yauzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akiangalia jinsi mfumo wa wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa unavyofanya kazi katika kutoa tarifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo.
Wadau mbalimbali wa vyakula na dawa wakifuatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa mfumo wa wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa uliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Binafsi nadhani hata ule utaratibu wa kununuwa dawa ambapo unapouziwa mbali ya maelezo uyapatayo toka kwa 'Pharmacist' jinsi ya kuzitumia dawa hizo, lakini unakuta siyo kuwa zote au hata kwa pengine ni asilimia kubwa huwa hazina 'leaflet' yeyote ndani yake au inayoambatana na dawa hizo, kwa pengine ingeweza kukupa maelezo ya kutosha kukhusu athari zake (side effects) ambazo kuna uwezekano wa kuweza kukutokea kutokana na matumizi ya dawa hizo husika na kwa pengine zingekupa dalili za awali kabisa kama ni kuendelea kuzitumia au kuziacha au hata kwenda kuonana na daktari haraka iwezekanavyo kabla athari hazijawa kubwa. Unakuta ni aina chache sana za dawa ziuzwazo kwenye maduka ya dawa mitaani, most of them huwa hazina kitu kama hicho (leaflet) na mathalan pia zikiwepo, basi bado kwa baadhi yetu ni tatizo, maana lugha inayotumika mara nyingi ni hizi lugha za kigeni (Kiingereza, kifaransa, kiarabu n.k.) si aghlab au hukuti kabisa zikiandikwa kwa Kiswahili . Kwa hiyo nadhani hilo nalo tukilifikiria na kulitafutia suluhu jinsi ya kuwaelimisha watumiaji wa dawa mbali mbali za binaadamu, pia litasaidia kuziepuka athari kadha wakadhalika zitokanazo na matumizi ya dawa hizo. Maana ukisoma 'leaflet' hizo, hakika utafahamu dawa husika zina matokeo gani na hivyo kukutowa khofu na kuwa makini katika kuweza kuzibaini athari zake mara moja endapo utakuwa 'allergy' nazo n.k. Kwani itakuwa ni vyema na salama zaidi na kuweza kuchukuwa tahadhari kabla ya khatari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...